Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hakimu agoma kujitoa kesi ya Zumaridi

Diana Bundala maarufu ‘Mfalme Zumaridi’

Muktasari:

  • Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Monica Ndyekobora anayeendesha kesi ya jina inayomkabili Diana Bundala maarufu ‘Mfalme Zumaridi’ amegoma kujitoa katika kesi hiyo kwa maelezo kuwa maombi ya mshtakiwa huyo anayetaka ajitoe hayana mashiko.



Mwanza. Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Monica Ndyekobora anayeendesha kesi ya jina inayomkabili Diana Bundala maarufu ‘Mfalme Zumaridi’ amegoma kujitoa katika kesi hiyo kwa maelezo kuwa maombi ya mshtakiwa huyo anayetaka ajitoe hayana mashiko.

Hakimu Ndyekobora ametoa uamuzi huo leo Jumatano Julai 27, 2022 huku akisisitiza kwamba kesi hiyo itaendelea kusikilizwa chini yake.

Baada ya kutoa uamuzi huo, hakimu aliitaka mahakama iendelee huku wakili wa Utetezi, Steven Kitale akisema upande huo hauoni sababu ya kuendelea na kesi hiyo na kuomba ipangiwe tarehe nyingine ili kutoa nafasi kwao kuanika sababu za kwa nini mteja wao amemtaka hakimu huyo kujiondoa katika kesi hiyo.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 10,2022.