Ghorofa laporomoka Dar, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya jengo moja la ghorofa lililopo Kariakoo Mtaa wa Congo na Mchikichi jijini Dar es Salaam kuporomoka.
Jengo hilo linaelezwa kuporomoka mapema leo Jumamosi Novemba 16, 2024. Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda, zinaeleza kuwa ndani ya jengo hilo la kibiashara, kulikuwa na watu kadhaa waliokuwa wakifanya ununuzi katika maduka ya jengo hilo.

Polisi kwa kushirikiana na wananchi wanaendelea na juhudi za uokoaji.
Zaidi aendelea kuifuatilia Mwananchi Digital.