Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GGML, Serikali yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani Juni 5, 2025, Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Serikali imeandaa matukio mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha jamii kushiriki katika utunzaji wa mazingira.

Maadhimisho hayo huadhimishwa kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa chini ya uratibu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ambapo kwa hapa nchini Tanzania shughuli mbalimbali zinazolenga kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira zimekuwa zikifanyika.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni “ Tokomeza uchafuzi wa plastiki kwenye mazingira ”.

Kwa mujibu wa Meneja wa Mazingira wa GGML, Yusuph Mhando, mwaka huu, maadhimisho ya siku ya mazingira yamehusisha ushirikiano kati ya Geita Gold Mining, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), uongozi wa serikali za mitaa, wadau wa elimu, vyombo vya habari, pamoja na sekta binafsi.

Amesema kuwa shughuli hizo zinahamasisha ushiriki wa jamii na vijana katika kuhifadhi mazingira, huku elimu ya mazingira na usafi wa jamii ikiwa katika kiini cha programu.

Shule za msingi za Nyakabale, Nyamalembo, Manga na Mgusu zinahusishwa katika shughuli za usafi na mafunzo ya mazingira kwa wanafunzi, zikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwajengea watoto uelewa wa masuala ya mazingira mapema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka GGML, katika kuleta hamasa zaidi, mjadala wa redio kupitia Storm FM umeandaliwa kwa kushirikisha maafisa wa serikali, wataalamu wa mazingira na wanajamii kujadili namna ya kushughulikia changamoto za mazingira katika ngazi ya jamii.

Vilevile, shughuli ya kufanya usafi katika Soko la Nyankumbu inalenga kuwahamasisha wafanyabiashara na wakazi kuhusu usafi wa mazingira na matumizi mbadala yenye kuleta endelevu katika mazingira.

Maadhimisho haya yatahitimishwa tarehe 5 Juni kwa mdahalo wa wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Kasamwa, ukijikita kwenye mada ya kutokomeza uchafuzi wa plastiki na mabadiliko ya tabianchi.

Shughuli hizi ni sehemu ya juhudi za kitaifa za kuunga mkono ajenda za kimataifa kuhusu mazingira, huku zikijengwa juu ya mafanikio ya miaka iliyopita, ikiwemo utekelezaji wa mradi wa maji katika Kijiji cha Nyakabale na utoaji wa vifaa vya usimamizi wa taka kwa Halmashauri ya Manispaa ya Geita.

Maadhimisho ya mwaka huu yanaenda sambamba na kumbukizi ya miaka 25 ya shughuli za GGML mkoani Geita, ikionyesha mwendelezo wa ushirikiano wake katika elimu ya mazingira na maendeleo endelevu ya jamii.