Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gari la wizi lasababisha kigogo wa Polisi kuvuliwa cheo

Muktasari:

Pia, jeshi hilo limemfukuza kazi kwa fedheha (kwa kutolipwa haki zozote) ofisa wake mwingine wa cheo cha Koplo, Federika Shirima anayetuhumiwa kukutwa na magari mawili yaliyoibwa jijini Dar es Salaam.

Moshi. Jeshi la Polisi limemvua cheo mkuu wake wa kituo cha Himo (OCS), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Zuhura Suleiman kwa tuhuma za kukutwa na gari la wizi aina ya Toyota Rav4.

Pia, jeshi hilo limemfukuza kazi kwa fedheha (kwa kutolipwa haki zozote) ofisa wake mwingine wa cheo cha Koplo, Federika Shirima anayetuhumiwa kukutwa na magari mawili yaliyoibwa jijini Dar es Salaam.

Hatua ya jeshi hilo dhidi ya askari wake imechukuliwa saa chache baada ya gazeti hili kufichua tuhuma hizo ambazo zilionekana kulipaka tope.

Habari zinazohusiana