Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Faru Rajabu afariki dunia

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Faru Rajabu alikuwa mtoto wa faru maarufu aliyejulikana kama Faru John aliyefariki mapema mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 47.

Dar es Salaam. Faru Rajabu amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 43.

Faru Rajabu alikuwa mtoto wa faru maarufu aliyejulikana kama Faru John aliyefariki mapema mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 47.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Pascal Shelutete inaeleza kuwa Faru Rajabu alifariki katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa ni uzee.

“Sirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) linasikitika kutangaza kifo cha Faru Rajabu wenye umri wa miaka 43 kilichotokea usiku wa kuamkia leo kutokana na sababu ya uzee katika Hifadhi ya Taifa Serengeti” imesema sehemu ya taarifa ya Tanapa

Kwa mujibu wa Tanapa mwili wa faru huyo utahifadhiwa kwa mujibu wa kanuni za asili za uhifadhi.

Faru Rajabu ambaye alizaliwa kwenye eneo Ngorongoro mwaka 1979 na mwaka 1993 alihamia katika Hifadhi ya Serengeti ameacha watoto, wajukuu na vitukuu kadhaa.

Kifo cha Faru Rajabu kimekumbusha kifo cha baba yake John alihamishwa maeneo kadhaa kutokana na tabia zake za ugomvi dhidi ya madume wengine zilizokuwa zikitishia uhai wake kwani alijeruhiwa mara kadhaa na Faru wengine na yeye kuwajeruhi.

Lakini baadaye Faru John alifariki na kuacha mtoto faru Rajabu ambaye anayejizolea umaarufu tofauti na tabia za baba yake, Faru Rajabu yeye anajitihada kubwa za kuongeza uzao wake.

Faru Rajabu ambaye aliwahi kupongezwa na hayati Rais John Magufuli amefanikiwa kuongeza idadi kubwa ya Faru katika eneo la ikolojia ya Serengeti na hata kufikia hatua Faru huyo, kuanza kuombwa kupelekwa katika hifadhi nyingine ili kuongeza Faru.


Kwanini Faru ni mnyama adhimu


Faru ni moja ya wanyama walio katika kundi la wanyama ambao wapo hatarini kutoweka duniani hivyo, ulipoibuka umahiri wa Faru Rajabu ilikuwa ni faraja katika uhifadhi za Faru sio Tanzania tu bali duniani .


Faru wapo hatarini kutoweka duniani kutokana na tishio la uwindaji haramu wa faru ambao wanajihusisha biashara ya pembe za faru licha ya kupigwa marufuku maeneo mengi.

Majangili wamekuwa wakiua faru ili kuchukuwa pembe zake zinatumika katika nchi za Asia kama tiba ya magonjwa mbalimbali na madai potofu kuwa kuboresha nguvu za kiume jambo ambalo kitaalamu linapingwa.

Biashara haramu ya pembe zao inachochewa na thamani kubwa ya pembe hizo ambapo kilo moja ni takriban Dola 65,000 ambazo ni zaidi ya Sh140 milioni.

Hata hivyo, kwa sasa Tanzania ni moja ya mataifa machache duniani, ambayo yanatajwa kufanikiwa sana kudhibiti ujangili wa faru na hivyo kusababisha kuongezeka kwa wanyama hao.