Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Exim, Tawen watoa elimu ya biashara kwa wajasiriamali Temeke

Benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN) wameendesha mafunzo ya biashara,  elimu ya fedha na mikopo kwa wajasiriamali wanawake waliopo wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam wakilenga kuwaandaa ili waweze kutumia vema mikopo, huduma na fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo, serikali pamoja na halmashauri ya wilaya hiyo.

Mafunzo hayo ya siku moja yaliyowakutanisha  pamoja wajasiriamali zaidi ya 450 kutoka wilayani humo yalifunguliwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Tawen, Janeth Mbene na kufungwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Munkunda.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo Munkunda pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa kudhamini na kushiriki moja kwa moja katika uwasilishaji wa mada mbalimbali kuhusu elimu ya mikopo, huduma za kibenki na matumizi ya fedha wakati wa semina hiyo, alisema  mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa wajasiriamali hao kutumia vyema mikopo wanayoipata kutoka kwenye taasisi za fedha,  serikali na halmashuri ya wilaya hiyo ili kujikwamua kiuchumi.

 “Licha ya jitihada kubwa inayofanywa na halmashauri yetu pamoja na taasisi za kifedha ikiwemo benki ya Exim katika kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali vikiwemo vikundi vya kina mama bado tumekuwa hatupati matokeo mazuri sana kwasababu wengi wa walengwa wamekuwa wakishindwa kutumia vema mikopo husika na matokeo yake wanashindwa kufikia malengo. Tunawashukuru sana TAWEN, Benki ya Exim na wadau wengine kwa kuona hili kwa kuwa semina kama hizi zinasaidia kuondoa changamoto hiyo,’’ alisema.

Aliwasihi wajasiriamali hao kuzingatia mafunzo hayo sambamba na kuendelea kuunda vikundi vitakavyowawezesha kunufaika zaidi na mikopo inayotolewa na serikali, halmashauri na taasisi mbalimbali za fedha huku akiwasisitiza kutumia muda wao mwingi kwenye shughuli zinazowaingizia kipato sambamba na kuwekeza muda katika malezi sahihi ya watoto badala kutumia muda mwingi kufikiria zaidi sherehe zinazowaingiza kwenye matumizi yasiyo na ulazima.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika semina hiyo Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim, Agnes Kaganda pamoja naye Mkuu wa Bidhaa za Rejareja na Uhakika wa Mapato wa benki hiyo, Mtenya Cheya walisema  ushiriki wa benki hiyo kwenye semina hiyo unalenga  kujenga uelewa wa kutosha kuhusu usimamizi bora wa kifedha, umuhimu wa huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo pamoja na namna bora ya kutunza akiba zao waweze kuendesha shughuli zao kitaalamu ili waepukane na hasara zinazoweza kukwamisha ustawi wa biashara zao.

“Katika mafunzo haya benki ya Exim pamoja na kuwa wadhamini tumejitahidi sana kuhakikisha walengwa wanajengewa uelewa wa kutosha kuhusu elimu ya kifedha sambamba huduma zetu zilizobuniwa mahususi kwa ajili yao ikiwemo akaunti ya ‘Supa Woman’ pamoja na akaunti ya ‘Wajasiriamali.’

“Huduma hizi zinalenga kurahisisha uendeshwaji wa biashara miongoni mwa wafanyabiashara wanawake na wafanyabiashara wadogo nchini kwa kuwawezesha kupata mikopo ya dharura ya hadi asilimia 90 ya kiasi kilichopo kwenye akaunti au hati fungani, mikopo ya nyumba na mikopo ya kawaida ya biashara. Zaidi pia kupitia akaunti yetu wa Supa Woman wateja wetu ambao ni wanawake wataweza kupata huduma ya bima ya maisha bure,’’ alibainisha  Kaganda.

Wakizungumzia mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Tawen, i Janeth Mbene pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo  Florence Masunga walisema mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa wajasiriamali hao katika kuwajengea uwezo wa kibiashara kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakishindwa kuendeleza vema biashara zao sambamba nakutumia vema mikopo wanayoipata kulingana na malengo kusudiwa.

“Changamoto kubwa kwa wajasirimali wanawake kama ilivyo kwa makundi mengine ni kukosekana kwa elimu ya kutosha katika uendeshaji wa shughuli zao hususani katika maeneo ya ukosefu wa elimu ya mikopo na elimu kuhusu fedha, kukosa washirika sahihi wa kibiashara, kukosa maeneo rasmi ya biashara na hata michango yao haitambuliki kitaifa licha ya wao kuwa na mchango mkubwa katika uendeshaji wa uchumi wa nchi kupitia biashara na kilimo,’’ alibainisha Mbene.