Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Elimu ya mikopo changamoto kwa wajasiriamali

Mmiliki wa Bright Future Academy ya Zanzibar, Dora Mathias Baliza akizungumza wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi ya SELF Zanzibar

Muktasari:

  • Kukosekana kwa elimu ya mikopo na biashara kumetajwa kuwa changamoto inayowapotezea fursa wajasiriamali na kuwafanya washindwe kurejesha na hatimaye kuathiri biashara.

Zanzibar. Kukosekana kwa elimu ya mikopo na biashara, kumetajwa kuwa moja changamoto inayowapotezea fursa wajasiriamali na kuwafanya washindwe kufanya marejesho, na hivyo kuathiri biashara zao.

Akizungumza katika ziara ya Bodi ya Mfuko wa fedha wa SELF, Meneja wa mfuko huo Zanzibar, Ramadhani Masebu, amesema kuwa kutokana na changamoto hizo, wameamua kutoa elimu kwa kuzifikia wilaya zote za Zanzibar, ili wateja wao watimize malengo ya wakopaji.

“Katika kuwafikia wajasiriamali wetu wadogo na wa kati, tunajitahidi sana katika kutoa elimu ya mikopo na elimu ya biashara na hili ni eneo muhimu sana.

“Tumeona tunapotoa mikopo ni lazima tutoe elimu ya ujasirimali na mikopo kwa manufaa ya watu wetu, lengo letu ni kuhakikisha tunawahudumia wajasirimali wote, wadogo, wa kati na hata wakubwa, kwani Mtanzania ana fursa kubwa ya kujikuza kiuchumi,” amesema.

Kwa upande wake Meneja Masoko na Uhamasishaji wa mfuko huo, Linda Mshana, amesema wamelenga kukidhi mahitaji ya mitaji kwa makundi mbalimbali Tanzania bara na visiwani.

“Kulingana na mahitaji na mikopo na kuongezeka kwa utitiri wa taasisi za mikopo, vijana wa kitanzania wanashauriwa kuungana na kukopa kwenye taasisi za fedha za kuaminika na zenye usimamizi wa Serikali ili kuepuka fedheka katika mikopo hiyo,” alisema.

Akizungumzia manufaa ya mikopo hiyo, Mkuu wa Shule ya Bright Future Academy iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi, Mwalimu Ibrahimu Julius amesema wao ni sehemu ya wanaufaika wa mfuko huo ambao unasimamiwa na Serikali.

“Tulinufaika na mkopo huu wa SELF kwani tulikabiliwa na uhaba wa madarasa kwa kiwango kikubwa,  tulikopa na kuongeza vyumba vya madarasa 17 na kufanya ongezeko la madarsa kutoka 14 hadi 31 na kwakweli tunayaona manufaa yake,” amesema.