Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Yonazi awafunda maofisa Tehama

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jim Yonazi akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa mawasiliano jijini Arusha. Picha na Happy Lazaro

Muktasari:

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi amewataka maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) nchini kuwa wabunifu na kujifunza ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia yanayojitokeza kila wakati.

Arusha. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi amewataka maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) nchini kuwa wabunifu na kujifunza ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia yanayojitokeza kila wakati.

Ameyasema hayo leo Jumanne Januari 25, 2022 jijini Arusha  katika kikao cha wadau wa mawasiliano Serikalini  kilichowahusisha wakurugenzi wa Tehama wa wizara zote na wakurugenzi wa rasilimali watu nchini cha kujadilii mahitaji ya taaluma ya Tehama yanayotekelezwa katika mradi wa Tanzania ya kidigitali.

Amesema kuwa, kutokana na mabadiliko ya teknolojia ya Tehama duniani kila wakati inahitajika kutoa mafunzo ya mara kwa mara kuongeza ujuzi ili kwenda na kasi ya mabadiliko hayo.

"Mafunzo haya yaende sambamba na mageuzi ya teknolojia na uharaka wake duniani kwa kujenga na kuongeza vituo vya malipo ya Serikali kwa njia ya kidigitali utakaosaidia wananchi kupata huduma hiyo popote walipo" amesema Dk Yonazi.

Mratibu wa mradi wa Tanzania ya kidigitali Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Honest Njau amesema  kuwa mradi huo unagharimu  Dola za kimarekani 150 milioni sawa na  fedha za kitanzania bilioni 349 na ulishaanza tangu mwaka jana ambapo utatekelezwa ndani ya miaka 5.

Amesema kuwa Serikali ipo mbioni kujenga minara ya mawasiliano mia nne ya kimkakati nchini ikiwa ni maboresho ya kuendana na matumizi ya internet hasa maeneo vijijini.

"Tupo mbioni kujenga zaidi ya minara 400 kutoka 2G kwenda 4G ili kuendana na kasi ya matumizi ya internet huko vijijini ambapo mawasiliano ya aina hiyo hamna na yanachelewesha ujenzi wa uchumi na maendeleo ya mawasiliano" amesema Njau

Imeandikwa na Happy Lazaro