Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Servacius Likwelile afariki dunia

Likwelile afariki dunia

Muktasari:

Katibu mkuu wa zamani Wizara ya Fedha, Dk Servacius Likwelile ambaye alikuwa mhadhiri wa idara ya uchumi Ndaki ya Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) amefariki dunia leo Jumamosi Februari 20, 2021.

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servasius Likwelile amefariki dunia leo Jumamosi Februari 20, 2021 jijini Dar es Salaam.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Vicky Kamata ambaye ni mke wa Dk Likwelile ameandika, “nilidhani mimi ni jasiri lakini kwa hili kumbe mimi si lolote, Mungu mbona umeniacha?”

Dk Likwelile aliyekuwa mchumi mwandamizi katika Ndaki ya Sayansi ya Jamii  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) aliteuliwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete kuwa katibu mkuu wa wizara hiyo kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais John Magufuli Agosti 31, 2016 na kumteua Dotto James.


Habari zaidi zitakujia hapa hapa katika tovuti yetu ya Mwananchi