Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mpango: Ni safu itakayofunga magoli siyo kubabaisha

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango.

Muktasari:

  • Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, yametajwa kama hatua ya kupanga safu ya ushindi wa magoli yasiyo ya kubabaisha.

Dar es Salaam. Hatua ya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan Agosti 30, mwaka huu, imetajwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango kuwa safu ya kufunga magoli.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo, juzi akiteuwa mawaziri wapya, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu, kadhalika aliwahamisha wengine kutoka katika nafasi zao za awali.

Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha wateule hao visiwani Zanzibar leo Ijumaa Septemba 1, 2023, Dk Mpango amesema kilichofanyika ni kupanga safu nzuri itakayowezesha kufunga magoli.

“Rais ameona ni vyema apange safu inayoweza kufunga magoli zaidi ili twende tukafunge magoli ya ukweli siyo ya kubabaisha,” amesema.

Mengine aliyoeleza katika hafla hiyo ni ushirikiano baina ya wateule hao, kadhalika wazingatie falsafa za kiongozi Mkuu (Rais Samia).

Katika hotuba yake hiyo, Dk Mpango amemtaja Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa kuwa na kibarua cha kutatua migogoro ya ardhi.

Lakini, kibarua kingine amesema ni kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki kutatua migogoro ya wananchi na hifadhi.