Dk Bilal azindua matembezi kuchangia fedha za Ukimwi

Dar es Salaam. Makamu wa Rais Mstaafu, Dk Mohamed Gharib Bilal (pichani) amezindua rasmi msimu wa 16 wa matembezi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha ili kusaidia mfuko wa kupambana na Ukimwi.
Akisoma risala yake jana jioni alipokuwa akizindua matembezi hayo, Dk Bilal amesema jitihada za kupambana na Ukimwi zinatia moyo kutokana na takwimu zilizopo.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa kwa 2010/2015 kiwango cha maambukizi ya mapya ya virusi vya Ukimwi kilishuka kwa asilimia 20.
Amesema jambo jingine linalotia faraja ni kuwa zaidi ya nusu wa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wamepata dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo (AR’VS).