Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dereva basi lililoua abiria saba, asomewa mashitaka 29

Muktasari:

  • Dereva huyo alifikishwa mahakamani hapo Aprili 23, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, Ally Mkama na kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashitaka wa Serikali, Julieth Komba.

Moshi. Dereva wa basi la Kampuni ya Mvungi Al-Adani Mruma, aliyesababisha ajali iliyoua watu saba na kusababisha majeruhi zaidi ya 42 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro na kusomewa mashitaka 29.

Ajali hiyo ilitokea Aprili 3, 2025 eneo la Kikweni, Kijiji cha Mamba, kata ya Msangeni, Wilaya ya Mwanga, mkoani humo baada ya basi hilo lililokuwa likitokea Ugweno kwenda jijini Dar es Salaam kupinduka kwenye bonde na kusababisha vifo vya watu saba na majeruhi 42.

Dereva huyo, alifikishwa mahakamani hapo jana Jumatano Aprili 23, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, Ally Mkama na kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashitaka wa serikali, Julieth Komba.

Miongoni mwa mashitaka anayokabiliwa nayo ni kusababisha vifo, kuharibu mali na kusababisha majeraha kwa abiria waliokuwa wakisafiria basi hilo.

Katika hati ya mashitaka iliyosomwa na mwendesha mashitaka mahakamani hapo, Julieth Komba aliieleza kuwa, shitaka la kwanza hadi la saba analoshitakiwa nalo mshitakiwa huyo ni kwamba aliendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya abiria saba akiwa dereva wa basi namba T 222 DNL, Yountong.

Aidha Komba, aliieleza mahakama hiyo kuwa, waliofariki katika ajali hiyo ni Halima Ramadhan, Hamadi Mshana, Zaituni Mwanga, Judith Mwanga, Benedetha George, Haji Mziray na Laila Mmary.

Shitaka la nane linalomkabili dereva huyo  ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa gari alilokuwa akiendesha mali ya Kampuni ya Mvungi,  huku shitaka  la tisa hadi 29 likiwa ni kuendesha gari kwa uzembe na  kusababisha  majeraha  kwa abiria waliokuwa kwenye basi hilo.

Mwendesha mashitaka huyo wa Serikali, aliileza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na hivyo akaiomba mahakama hiyo kupanga tarehe ya kuanza kusomewa maelezo ya awali (PH).

Hata hivyo, baada ya mshitakiwa huyo kusomewa maelezo hayo alikana kusababisha makosa hayo.

Hakimu Mkama alimweleza mshtakiwa kuwa kwa mujibu wa sheria makosa hayo ni miongoni mwa makosa ambayo yanadhamana ambapo masharti ni  kuwa na wadhamini wawili wenye mali zisizohamishika zenye thamani ya Sh10 milioni,  barua za utambulisho na vitambulisho.

Mshtakiwa huyo alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kupelekwa gerezani na kesi hiyo iliahirishwa mpaka Aprili 25, 2025.