Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Ludewa ataka kesi zimalizwe kwa usuluhishi

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amewahimiza wananchi kutatua migogoro kwa njia za usuluhishi.

Ludewa. Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amewataka wananchi wilayani humo kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ili kuokoa muda wa kufanya shughuli za kimaendeleo.

 Ameyasema hayo leo Februari Mosi wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Mwanziva amesema kutatua changamoto kwa njia ya usuluhishi kunasaidia kupata haki kwa wakati ka kuokoa muda wa kufanya kazi za maendeleo.

“Kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kunasaidia wananchi kutafuta maendeleo kuliko kutafuta haki mahakamani kwa sababu mahakamani kuna hatua nyingi za kupitia,” amesema Mwanziva.

Amesema ucheleweshwaji wa haki ni moja ya sababu za ucheleshwaji wa maendeleo nchini, hivyo amewataka wananchi kudumisha njia ya usuluhishi.

Kwa upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Isaac Ayeng’o amewataka wajumbe wa mabaraza ya usuluhishi kuepuka kuwa na masilahi kwenye migogoro ili haki itendeke.

Ameongeza kuwa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi husaidia kutunza faragha za wahusika.

“Wadau lazima tuweke mazingira mazuri ya usuluhishi, husaidia kutunza faragha kuliko kusimama kwenye mahakama ya wazi ambako kila kitu kilichotendeka kitawekwa wazi na wote watajua,” amesema Ayeng’o

Naye Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Mathan Chalamila ameyataka mabaraza ya kata kuzingatia miongozo ya utatuzi wa migororo ili haki ipatikane kwa wakati bila ya kufikishana mahakamani.