Dawasa yatangaza upungufu maji Dar, Bagamoyo

Muktasari:
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) imesema kuwa kutakuwa na upungufu wa maji katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) imesema kuwa kutakuwa na upungufu wa maji katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo.
Taarifa iliyotolewa na Dawasa imesema kuwa upungufu huo utakaoanza leo Alhamisi Aprili 14, 2022 hadi kesho unatokana na kujaa tope katika machujio ya maji kwenye mtambo wa mto Ruvu kutokana na mvua zinazonyesha mkoani Morogoro.
Taarifa hiyo imesema kua Kiwango cha uzalishaji maji kitapungua kwa asilimia 25, hivyo msukumo wa maji utakuwa mdogo kwenye maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini.
Maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo ambayo yataathirika ni pamoja na; Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo, Kikuu na Mwenge.
Mengine ni Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya mji.