Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Darasa la saba zaidi ya nusu wapata ‘D’ hisabati

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohamed

Muktasari:

  • Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya darasa la saba 2023 huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 0.96. Pia matokeo hayo yameonyesha kushuka kwa ufaulu katika somo la hesabu.

Dar es Salaam. Matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 13-14, 2023 yametangazwa leo Alhamisi Novemba 23, 2023 na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) huku ufaulu ukiwa mbaya katika somo la hisabati

Akitangaza matokeo hayo mbele ya wanahabari katika ofisi za Baraza hilo, jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohamed amesema mbali na matokeo hayo ufaulu wa somo la Hesabu umeshuka kwa asilimia 4.46 ikilinganishwa na mwaka jana.

"Ufaulu somo la hisabati umeshuka kutoka asilimia 52 mwaka jana hadi asilimia 48.83 mwaka huu, kwani asilimia 51 ya watahiniwa wote wamepata daraja D," amebainisha.

Hata hivyo, ufaulu kwa ujumla umeongezeka kutoka asilimia 79.62 mwaka 2022 hadi 80.58 mwaka huu sawa na asilimia 0.96.

Necta imesema jumla ya watahiniwa 1,092,960 sawa na asilimia 80.58 ya watahiniwa 1,356,296 wamefaulu kwa kupata daraja A, B na C.

Mbali ya kuongezeka kwa ufaulu, matokeo hayo yameonyesha uwiano sawa wa ufaulu huo kati ya wavulana na wasichana ambapo wavulana waliofaulu ni 507,920 sawa na asilimia 80.59, huku wasichana wakiwa 585, 040 sawa na asilimia 80.58.

Akizungumzia matokeo yaliyozuiliwa, Dk Mohamed amesema baraza limezuia matokeo ya watahiniwa 360 waliopata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

"Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kurudia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2024 kwa mujibu wa kifungu cha 32(1) cha kanuni za mitihani.

Hata hivyo, amesema baraza limefuta matokeo yote ya watahiniwa 31 nchini sawa na asilimia 0.002 ya watahiniwa waliofanya mtihani ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika mtihani.

Vilevile, Dk Mohamed ameeleza kuwa baraza limefungia vituo viwili vya mtihani ambavyo ni Twibhoki na Graiyaki vya halmashauri ya Serengeti mkoani Mara.

"Vituo hivyo vimethibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mtihani vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu 4(8) cha kanuni za mtihani mwaka 2016 mpaka hapo Necta itakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya Taifa," ameeleza.