Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dar yatengewa Sh260 bilioni kurekebisha barabara mbovu

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Josephat Kandege akijibu maswali ya wabunge katika kikao 17 cha mkutano wa 15 bungeni jijini Dodoma leo. Picha na Ericky Boniphace

Muktasari:

  • Katika kuhakikisha biashara na huduma zinaendelea kama kawaida jijini Dar es Salaam, Serikali imetenga mabilioni ya fedha kukarabati barabara zilizoharibika kutokana na sababu mbalimbali jijini humo

Dodoma. Kutokana na umuhimu wa miundombinu ya usafiri na uchukuzi jijini Dar es Salaam, Serikali imetenga Sh260 bilioni kukarabati barabara zilizoharibika kutokana na sababu mbalimbali jijini humo.

Pamoja na ukarabati huo utakaoanza muda wowote kuanzia sasa, naibu waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege amesema taa 5,000 za barabarani zimefungwa jijini humo ili kuimarisha ulinzi wakati wa usiku.

Kandege amesema hayo bungeni leo Ijumaa Mei 3 alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum (Chadema), Antropia Theonest aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kushughulikia changamoto ya ukosefu wa madaraja katika barabara za jimbo la Segerea.

“Serikali imesaini kandarasi ya Sh260 bilioni kukarabati barabara ba miundombinu iliyoharibika jijini Dar es Salaam ambako tayari kumefungwa taa 5,000 za barabarani,” amesema Kandege.

Anatropia pia alitaka kujua Serikali inafanya nini kumaliza kero ya ukosefu wa madaraja katika jimbo hilo ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 15. Vilevile, alitaka kujua lini barabara ya Segerea Sheli kwenda Kipawa kupitia Seminari itaanza kujengwa.

Akijibu kuhusu barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2.93, Kandege amesema ipo chini ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) Manispaa ya Ilala na ilishafanyiwa usanifu.  

“Barabara hii inapita katika Mto Msimbazi mbako hakuna daraja. Changamoto iliyopo ni kutanuka kwa mto huo hivyo kuhitaji ‘study’ (uchambuzi) ya kina na mapitio ya usanifu ili kupata mahitaji halisi ya ujenzi wa daraja hilo,” amesema Kandege.