Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chongolo amtaka Bashungwa kukamilisha barabara Katavi

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akizungumza na wanachama, viongozi wa CCM wa Mpanda Mjini, Jumatatu Oktoba 2, 2023 katika ofisi za chama hicho mkoani Katavi. Picha na Mpiga Picha wetu

Muktasari:

  • Barabara hiyo ya Kibaoni-Mlele yenye urefu wa kilomita 50, Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi inayojengwa na mkandarasi ya M/s China Railway Seventh Group Co.Ltd (CRSG) kwa gharama ya Sh88.7 bilioni kwa muda wa miezi 36.

Katavi. Kusuasua kwa ujenzi wa barabara ya Kibaoni-Mlele kilomita 50, Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi na malipo kwa mkandarasi, yamemfanya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kutoa maagizo kwa wahusika akiwemo Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa.

Amemtaka Waziri Bashungwa kufika mkoani humo Jumamosi hii akiwa na majibu yakinifu ya utekelezaji wa mradi huo na kuitaka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuwalipa wakandarasi kwa mujibu wa taratibu ili kutoiongezea gharama Serikali zinazoepukika.

Ametoa maagizo hayo leo Oktoba 4 wakati akikagua barabara hiyo inayojengwa na mkandarasi ya M/s China Railway Seventh Group Co.Ltd (CRSG) kwa gharama ya Sh88.7 bilioni kwa muda wa miezi 36 kuanzia Juni 23 mwaka jana na unapaswa kumalizika Juni 22, 2025.


Chongolo na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya chama hicho, Issa Ussi Gavu wako mkoani Katavi kwa ziara ya siku tano kuanzia juzi hadi Oktoba 7, kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25 na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Maagizo hayo yalitokana na taarifa ya Kaimu Meneja wa Tanroads, Mkoa wa Katavi, Albert Laizer aliyeelezea utekelezaji wa mradi huo ambao barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Tunduma- Sumbawanga-Mpanda- Kanyani mkoani Kigoma.

Laizer aliseema mradi umefikia asilimia 11.2,"ukiwa umeanza kuwa nyuma ya ratiba ya utekelezaji kwa vile utekelezaji ulipaswa kuwa umefikia asilimia 21. Muda wa utekelezaji umefikia miezi 15 kati ya 36."

Alisema hadi sasa Serikali imekwisha kumlipa mkandarasi malipo ya awali Sh12.93 bilioni. Hata ya malipo ya kwanza iliidhinishwa Sh4.12 bilioni na muda wa mkataba unapaswa kuwa Oktoba 2 mwaka huu lakini amelipwa Sh1 bilion.

Laizer amegusia changamoto ya mradi huo alisema ukiondoa, "changamoto ya mkandarasi kutofuata ratiba yake aliyojipangia kiasi cha kuwa nyuma ya utekelezaji, ana unaupungufu wa mahitaji ya vifaa vya ujenzi."

Baada ya taarifa hiyo, Chongolo alimuuliza shida ni nini hadi barabara hiyo inasuasua, Mhandisi Mkazi, Jovin Ndyetabula alisema,"tumekwisha kukaa nae mkandarasi na kumweleza aangalie ratiba yake na kuongeza kasi ya ujenzi."

Wakati akitembelea barabara hiyo, Chongolo alionesha kutoridhishwa na kumweleza Meneja Mradi wa CRSG, Nin Rwi kuwa "tunachokitaka ni kuongeza kasi ya ujenzi na si vinginevyo" huku meneja hiyo akimweleza atafanya hivyo.

Mara baada ya ukaguzi, Chongolo alikwenda kuzungumza na wananchi wa Kibaoni ambapo, Mwenyekiti wa CCM, Iddi Kimanta alisema,"kama ulivyoona, ujenzi unasuasua, mwezi ujao mvua zitaanza na kasi ya mkandarasi kama hii."

"Tunaomba kwa nafasi yako uweke msukumo na barabara hii ili iweze kukamilima na kuwaondolea adha wananchi," amesema Kimanta huku akishangiliwa na wananchi.

Ulipowadia wasaa wa Chongolo kuzungumza pamoja na mambo mengine alimtaka Waziri Bashungwa kufika mkoani humo kabla ya Jumamosi ambapo atahitimisha ziara hiyo kwa kufanya mkutano wa hadhara Mpanda Mjini.

"Nimeona ujenzi wa barabara, mwenyekiti wangu wa mkoa ameongea, kwa kweli sijaridhishwa sana na ujenzi wa barabara, alipaswa kuwa zaidi ya asilimia 40 lakini yuko asilimia kumi na kidogo, hili halikubalili," alisema Chongolo

Alisema amewataka wahusika wakutane akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga wapitie ratiba ya utekelezaji wa mradi huo,"hii najua wewe mkuu wa wilaya ni kijana, utaliweza.

"Lakini nimemwita waziri mwenyewe wa ujenzi (Bashungwa) aje hapa atuambie utekelezaji wa hili na baada ya hapo mtaona mabadiliko," alisema Chongolo

Katika kusisitiza hilo, Chongolo amesema,"waziri asipokuja atakuwa anajitafutia balaa, atakuja kutuambia na kabla ya kuja kwenye mkutano tarehe 7 Mpanda Mjini, aje kwanza huku kuongea na watu wake."

Pia, Chongolo amesema,"kuna wale walipewa dhamana ya kusimamia na kutoa fedha hasa Tanroads, tabia ya kuwa wanachelewesha malipo halipaswi kuendelea kwani kuchelewa ni kuongeza mzigo kwa Serikali na sisi kama chama hatuwezi kukubali hili likaendelea."