Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

China yaongoza kwa miradi yenye thamani kubwa Tanzania

Muktasari:

Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania (TIC) kimesema nchi ya China umeongoza kwa kuwekeza miradi yenye thamani kubwa nchini huku Uingereza ikiongoza kwa idadi kubwa ya miradi na utoaji wa ajira.

Dodoma. Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania (TIC) kimesema China inaongoza kwa kuwekeza miradi yenye thamani ya Dola 7,496.97 milioni za Marekani nchini kuanzia mwaka 1990  hadi Oktoba, 2020.

Hata hivyo, Uingereza inaongoza kwa kuwa na miradi mingi na kutoa ajira nyingi katika nchi zilizowekeza kwenye kipindi hicho.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Desemba 2, 2020 na mkurugenzi mtendaji wa TIC, Dk Maduhu Kazi katika kikao cha watendaji wakuu wa taasisi zinazotoa huduma kwa wawekezaji.

Kikao hicho kililenga katika kujadiliana namna bora ya kuboresha utoaji huduma kwa wawekezaji, utoaji vibali, vyeti, leseni kwa wakati kama ilivyoagizwa na Rais John Magufuli wakati akizindua Bunge Novemba 13, 2020.

Dk Kazi amesema China imewekeza miradi 940 na kutoa ajira 117,810 huku Uingereza ikiwekeza miradi 944 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 5,405.92 na kutoa ajira 274,330.

Dk Kazi amesema Marekani inafuatia kwa kuwa na miradi 244 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 4,740.79 na ajira 52,489.

Ameitaja nchi ya nne kwa uwekezaji wenye thamani kubwa katika kipindi hicho kuwa ni Mauritius kwa kuwekeza Dola za Marekani milioni 4,607.65 ikifuatiwa na India (Dola 3,553.17 milioni), Australia (Dola1,866.10 milioni), Kenya (Dola1,715.02 milioni),  Uholanzi (Dola1,051.02 milioni), Ubelgiji (Dola905.56 milioni) na Misri (Dola888.65 milioni).

Amesema jumla ya miradi iliyowekezwa na nchi hizo 10 ni 3625, na kutoa ajira  578,866 na thamani ya miradi hiyo ni Dola za Marekani milioni 32,251.51.