Charles Hilary ateuliwa Msemaji Mkuu Zanzibar

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amemteua Charles Hilary kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali.
Awali kabla ya uteuzi huo, Hilary ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu, Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Februari 6, 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema uteuzi umeanza leo.
Hata hivyo, cheo hicho hakikuwapo kwa sasa ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tangu utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk Salmin Amour Juma.