Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chanzo cha migogoro ya ardhi Pwani chatajwa

Muktasari:

Kwa sasa mkoa huo unakadiriwa kuwa na ng'ombe 505,788 wakati eneo la malisho lililotengwa ni hekta 498,001 ambalo lina uwezo wa kuchukua mifugo hiyo 249,002 tu.

Pwani. Chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji katika Mkoa wa Pwani kimeelezwa kuwa ni uwepo wa ziada ya ng' ombe 256,788 tofauti na uwezo wake.

Kwa sasa mkoa huo unakadiriwa kuwa na ng'ombe 505,788 wakati eneo la malisho lililotengwa ni hekta 498,001 ambalo lina uwezo wa kuchukua mifugo hiyo 249,002 tu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo kilichoketi mchana huu mjini  Kibaha.

"Migogoro ya wakulima na wafugaji mkoani kwetu inashika kasi siku hadi siku na inaendelea kuwa tishio kubwa la amani na utulivu wa jamii hizi mbili na chanzo chake tumebaini uwepo wa ziada ya ng'ombe 256,788 ndiyo inayoleta tafrani katika maeneo mbalimbali ya mkoa wetu" amesema mhandisi Ndikilo.

Akiwasilisha mada ya migogoro ya wafugaji na wakulima Katibu tawala msaidizi  Uchumi na uzalishaji Mkoani humo, Shangwe Twamala amesema kwa Pwani migogoro hiyo ilianza mwaka 2006 Serikali ilipoagiza wafugaji kutoka bonde la Ihefu Mbeya wahamishiwe mikoa ya Pwani,Lindi na Mtwara.

Twamala amebainisha kuwa mifugo hiyo iliongezeka wengi ni ng'ombe kutoka 148,099 mwaka 2005/ 2006 hadi 505,788 mwaka 2014/ 2015 ilipofanyika sensa maalumu ya mifugo na halmashauri zilijitahidi kutenga maeneo jumla ya hekta 498,000 na kutosha ng'ombe 250,000 tu kati ya 505,788 zilizotambuliwa.