Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chande atetea JNHPP kulinda mazingira

Muktasari:

Mkurugenzi Mkuu waTanesco, Maharage Chande amesema katika utekelezaji wa wa mradi wa Bwawa wa Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), Serikali ilizingatia na inafuata masharti ya ulinzi wa mazingira ya kimataifa.


Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema katika utekelezaji wa wa mradi wa Bwawa wa Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), Serikali ilizingatia na inafuata masharti ya ulinzi wa mazingira ya kimataifa.


Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 21, 2022 wakati wa mjadala wa Mwananchi- Twitter Space chini ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kuhusu umuhimu wa bwawa hilo kiuchumi.


Chande amesema kidunia, nchi za Afrika ndio zinazochangia uharibifu wa mazinmgira kwa kiasi kidogo.


“Lakini sisi ndio tunaopata athari za mazingira kuliko hao walioendelea.


“Tanzania sio mara ya kwanza kujenga mabwawa, tumejenga Mtera, Bwawa la Kihansi… kwa hiyo lazima ufanye uchambuzi wa kimazingira na baadaye uweke mpango wa kufidia athari hizo, tulizingatia hilo na mipango inatekelezwa. Tunaripoti kwenye vyombo kidunia kila wakati,”


Awali akizungumza katika mjadala huo, Robert Muganzi, Ofisa Mwandamizi wa Miradi katika mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka Taasisi ya Aga Khan (AKF) amehoji athari za ukataji wa miti bila mpango wa kurudisha, akitolea mfano wa gharama za ukuzaji wa mkoko mmoja kwa mwaka unaoweza kufyonza angalau kilogramu tatu za hewa ya ukaa.


Hoja nyingine iliyoibuliwa ni kuhusu uwezekano wa kushuka kwa bei za umeme baada ya kukamilika bwawa hilo la umeme ili kuchechemua shughuli za kiuchumi na kuongeza unafuu kwa wananchi.


Kuhusu bei za umeme, Chande amesema gharama zinaweza kushuka kutokana na mahesabu ya wakati huo wa uzalishaji, huku akifafanua namna Serikali ilivyopunguza gharama za umeme kwa wananchi kupitia gharama mbalimbali ikiwamo nguzo na kwamba iko chini kuliko nchi za Afrika mashariki.


“Bei ya kuunganishia umeme kwa wastani ni asilimia 50 chini ya gharama halisi za kuunganishia watu umeme, kwa hiyo, bwawa likianza tutakuwa na chanzo kingine gharama kushuka, itategemeana na mahesabu yetu, tusiweke matumaini.”