Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chadema: Msaidizi wa Lissu apatikana akiwa na pingu mkononi

David Jumbe akiwa na pingu akiripoti kituo cha Polisi Osterbay Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, Amani Golugwa amesema David Jumbe, msaidizi wa mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu amepatikana akiwa na pingu mkononi.

Amesema taarifa hizo amezipata hivi punde kutoka kwa mke wa Jumbe ambaye amethibitisha mumewe kurejea nyumbani akiwa na pingu mikononi.

David Jumbe akiwa na pingu akiripoti kituo cha Polisi Osterbay Dar es Salaam

Golugwa amesema Jeshi la Polisi waliofika makao makuu ya Chadema leo Alhamisi, Mei 21, 2026  saa tatu asubuhi walijitambulisha wanatoka kituo cha Polisi Oysterbay na wanamtafuta Jumbe ambaye walidai alitoweka na pingu.

Kwa mujibu wa Golugwa, askari hao wamedai Jumbe alijificha ndani ya Ofisi za  Chadema hivyo wanamtaka wamfungulie pingu.

"Tunawaambia Polisi Jumbe yupo nyumbani kwake waende kumfungulia pingu," amesema Golugwa.

Awali, taarifa zilizosambaa mitandaoni zilieleza David anadaiwa kuchukuliwa nyumbani kwake Mabwepande, Bunju jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Alhamisi. Taarifa hiyo inayodaiwa kuwa ni maelezo ya mke wa Jumbe ilisema:

“Jumbe alikuwa anarudi nyumbani na alipofika getini alifuatwa na watu hao, wakamkamata na kumwingiza kwenye gari aina ya Land Cruiser kisha kuondoka kwa mwendo mkali.


“Jumbe alipiga kelele na kujaribu kujitetea lakini watu hao wakamzidi nguvu. Majirani walipofika walijaribu kuikimbiza gari hiyo bila mafanikio,” imeeleza taarifa hiyo.

Katika purukushani hizo, Jumbe anadaiwa kudondosha kiatu alichokuwa amevaa kabla ya kuchukuliwa na watu hao ambao hawakujitambulisha kwa familia.

David Djumbe, msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu akiwa na pingu wakati akiripoti kituo cha Polisi Osterbay Dar es Salaam.

Mwananchi inaendelea kumsaka Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, kwa ufafanuzi kuhusu tukio la kuhojiwa kwa Golugwa na madai ya kutoweka kwa David Jumbe.