Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yajipanga mapokezi ya Dk Tulia

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Ndele Mweselela akizungumza na Mwananchi digital leo ofisini kwake jijiji Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela amesema leo Ijumaa, Novemba 10, 2023 wakati akizungumza na Mwananchi Digital kuhusiana na mapokezi ya Rais wa 31 Umoja wa Mabunge   Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson kesho Novemba 11 mwaka huu.

Mbeya. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimeandaa mapokezi makubwa ya Rais wa 31 wa  Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na  Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson huku kikieleza ushindi wa nafasi hiyo umetengeza demokrasia na sifa kwa Taifa la Tanzania

 Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaaa, Novemba 10, 2023 Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela amesema kama Mkoa wanajivunua ushindi wa Dk Tulia na  kwamba amethibitisha kupokea baraka za Rais Samia Suluhu Hassan kuwakilisha vyema kupeperusha bendera ya Tanzania.

“Tumshukuru Rais kwa kumteua Dk Tulia kushiriki kwenye kinyang'anyiro cha Uraia wa IPU amethibitisha uwepo dipromasia ya nchi   na matunda makubwa ya kuweka muundo mzuri wa Taifa,” amesema.

Mwaselela amesema Dk, Tulia ameonyesha uwezo wake mkubwa wa kuaminika ndani na nje ya nchi, kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kumtunza kumuunga mkono na kumpa ushiriano sasa Mbeya itazungumzwa kimataifa,”amesema.

 Amesema ni wakati wa Mungu ulifika kwa zamu ya nchi za Afrika, baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumpendekeza Dk Tulia kwa baraka zake kushiriki nafasi hiyo na kupata ushindi wa  kishindo dhidi ya wapinzani wake watatu na kuonyesha uwezo mkubwa  wa kukubalika ndani na nje ya mataifa mengine licha ya kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini.

“Dk Tulia ni mtoto wa CCM ni vyema tunapoona mambo makubwa anayofanya katika kuheshimisha  wanambeya  na Taifa kwa ujumla kwani uwepo wake utatengeza fursa za uwekezaji kwenye nyanja mbalimbali za kiuchumi sambamba na suala zima la ajira”amesema.

Mwaselela amesema kuwa katika mapokezi hayo ngazi ya Mkoa wanatarajia kupokea wageni mbalimbali sambamba na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.

“Niwakaribishe sana wananchi, wafanyabishara, bodaboda, kujitokeza kwa wingi kumpoke Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson ambaye tangu achaguliwe anaingia jimboni kwa mara ya kwanza,”amesema.

Ofisa Uhusiano na mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema wamejipanga kikamilifu katika mapokezi ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dk Tulia Ackson.

“Kimsingi mapokezi yatakuwa makubwa sana katika nyanja mbalimbali wakiwepo mama ntilie, bodaboda, bajaji, na nyanja nyingine kwa wanambeya  na kwamba kitendo cha kupenya katika nafasi hiyo nyeti ya  juu itatengenza fursa za uwekezaji wa ndani na nje,”amesema.

Katika hatua nyingine Mwakanolo amesema kuwa watanzania watarajie kuona mambo makubwa ya fursa za kiuchumi na kwamba Mkoa wa Mbeya unakwenda kuwa maendeleo ya kimkakati katika uwekezaji wa kiuchumi.

Mama lishe, Neema Solomon amesema wamejipanga kikamilifu katika mapokezi hayo, kwa lengo la kumuunga mkono Rais wa umoja wa mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini, Dk Tulia Ackson kwani amewaheshimisha wanambeya.

“Mbeya imebeba heshima kubwa, tunajivunia uwepo wake, pia tunamuomba Mungu ampe  maisha marefu ili andelee kupeperusha bendera ya Taifa na kumuheshimisha Rais Samia Suluhu Hassan ndani na nje ya nchi ya Tanzania,” amesema.