Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM Tanga yawaonya wanasiasa dhidi ya kauli za uchochezi 

Mwenyekiti wa CCM mkaoa wa Tanga, Rajabu Abdallah akiongea na waandishi wa habari kusisitiza suala la amani kwenye Sikukuu ya Eid El Fitri na kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Muktasari:

  • CCM Mkoa wa Tanga imetangaza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kitaanza rasmi harakati zake za kisiasa kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

Tanga. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdallah, amewataka wanasiasa wa ndani na nje ya mkoa huo kuhakikisha wanalinda amani kwa kuepuka siasa zenye viashiria vya uchochezi na uvunjifu wa amani. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi, Machi 29, 2025, wakati wa kutoa salamu za Sikukuu ya Eid El-Fitr, Abdallah amesema wananchi wanapaswa kuendeleza matendo mema waliyofanya katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuepuka kushawishiwa na makundi mbalimbali, hususan ya kisiasa. 

Amesema wapo baadhi ya wanasiasa wanaotumia matukio kama sikukuu kujinadi kisiasa, jambo ambalo wakati mwingine huweza kusababisha uvunjifu wa amani. Ameonya kuwa chama hicho hakitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo. 

Katika hatua nyingine, Abdallah ametangaza kuwa CCM itaanza rasmi shughuli zake za kisiasa mara baada ya Ramadhani ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. 

"Nawaomba wanachama wa CCM kuwa tayari kwa harakati za kisiasa. Tukimaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, chama kitaingia kazini bila mapumziko hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika," amesema. 

Aidha, amewakumbusha wanasiasa wote wanaotarajia kufanya shughuli zao mkoani humo kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni za nchi ili kuepusha migogoro inayoweza kusababishwa na kauli zao. 

Wakati huo huo, Abdallah amewapongeza wafanyabiashara wa bidhaa za futari mkoani Tanga kwa kuweka bei rafiki, hali iliyosaidia kupunguza malalamiko ya kupanda kwa bei ya bidhaa katika kipindi cha Ramadhani.