Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bujora yaomba kibali umiliki nyara za Serikali

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni na Maonyesho wa Wasukuma Bujora kilichopo Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza, Anania Mukanzabi akizungumza leo. Picha na Mgongo Kaitira

Muktasari:

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni na Maonyesho wa Wasukuma Bujora kilichopo Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza, Anania Mukanzabi  amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutoa kibali kwa kituo hicho kumiliki nyara za Serikali.

Mwanza. Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni na Maonyesho wa Wasukuma Bujora kilichopo Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza, Ananias Mukanzabi  amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutoa kibali kwa kituo hicho kumiliki nyara za Serikali.

Akizungumza leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Sherehe za Utamaduni wa Wasukuma na Ekaristi Takatifu (Bulabo), Padri Mukanzabi amesema ukosefu wa nyara hizo ikiwemo Nyoka, Fisi na ngozi za wanyama mbalimbali ni miongoni mwa changamoto zinazoikikumba kituo hicho.

Amesema changamoto nyingine kuwa ni gharama kubwa za maandalizi ya tamasha hilo huku akisema kituo hicho kinategemea michango ya watu jambo linalohatarisha ufanisi katika maandalizi yake kwa miaka ijayo.

"Maandalizi ni gharama kubwa kituo kinategemea michango ya watu mbalimbali na binafsi ikiwemo makampuni ya biashara, ambayo yalijiondoa katika udhamini. Tunapata wasiwasi iwapo tamasha hilo litaendelea kwa ufanisi katika miaka ijayo," amesema Padri Mukanzabi

Padri Mukanzabi ameishukuru Serikali kwa kutimiza ahadi yake ya kujenga barabara inayotoka Kisesa kwenda kilipo kituo hicho kwa kiwango cha lami na kuwekea taa jambo alilotaja kuwa limeboresha mazingira kuzunguka makumbusho hiyo.

Akitoa historia ya kituo cha Bujora, Padri Mukanzabi amesema kituo hicho kilizinduliwa rasmi mwaka 1972 na Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania, Hayati Julius Nyerere ambapo imekuwa sehemu muhimu ya kutunza, kuendeleza na kunadi tamaduni za kabila la Wasukuma.

"Ni moja ya makumbusho ya kipekee nchini eneo hili lina sehemu tano ambazo ni makumbusho, uongozi wa kisukuma, makazi ya wasukuma, uganga wa tiba asilia na sehemu inayotunza vifaa mbalimbali vya michezo," amesema Mukanzabi