Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brela yajitenga madai ya Kalynda kutapeli

Muktasari:

  • Wakati Watanzania wakiendelea kupaza kilio chao, kutapeliwa fedha zao na Kampuni ya Kalynda E-Commerce Limited inayojishughulisha na biashara mtandao, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema  kampuni ilipewa leseni ya uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielectroniki na mawasiliano kwa njia mtandao.




Dar es Salaam. Wakati Watanzania wakiendelea kupaza kilio chao, kutapeliwa fedha zao na Kampuni ya Kalynda E-Commerce Limited inayojishughulisha na biashara mtandao, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema  kampuni ilipewa leseni ya uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielectroniki na mawasiliano kwa njia mtandao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 12,Mwaka huu, Brela  imekiri kuifahamu kampuni hiyo lakini kufanya  biashara ya Upatu “Pyramid Business” ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda fulani  ni kinyume na bidhaa au huduma iliyoombewa na kupata leseni.

“Kampuni ya Kalynda E-Commerce Limited ilisajiliwa tarehe 14 Juni, 2022 na kupewa cheti cha usajili Namba. 156483877. Kwa mujibu wa katiba ya kampuni (Memorandum and Articles of Association) shughuli kuu za kampuni ni pamoja na uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielectroniki na mawasiliano, ufanyaji wa biashara ya kitekinolojia ya kimataifa mtandaoni,”imesema

Taarifa hiyo ilitolewa na Brela kupitia kitengo cha mawasiliano kwa umma imesema “wakati wa uwasilishaji wa maombi ya usajili wa Kampuni na Leseni ya Biashara taarifa zilizowasilishwa zilionesha ofisi ya Kalynda E-Commerce Limited zipo Kiwanja Na. 9, Mtaa wa Kaunda, Kata ya Msasani Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam,”.

Wakati Brela wakieleza hayo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema taarifa za utapeli huo wanaziona kwenye mitandao ya kijamii na kwamba hakuna mtanzania aliyeenda kuripoti kwenye ofisi hizo.

“Na sisi tunasikia na kuona kwenye mitandao hakuna mwananchi aliyekuja kuripoti kwenye ofisi zetu kwamba ametapeliwa na Kampuni hiyo unayonieza mwandishi kwahiyo wakifika na tukapokea malalamiko yao tutaanza kufanya uchunguzi,”amesema Kamanda Jumanne Muliro

Wahanga waliotapeliwa

Baadhi ya wahanga wa Kampuni hiyo wanadai Serikali kupitia taasisi zake hawawezi kukwepa kubeba mzigo wa lawama hizo kwani matangazo ya kampuni hiyo kufanya biashara hiyo yalikuwa yanarushwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vikubwa na wao waliamini na wakajiunga.

“Brela walipaswa kufuatilia kujua kama kazi walizokuwa wanafanya zinazingatia miongozo waliyopewa, haiwezeni Watanzania zaidi ya 100,000 alafu wanakuja kutoa ufafanuzi kwamba walikuwa wanafanya biashara kinyume na leseni waliyopewa,”anasema Shazima Hamis mkazi wa Babati mkoa wa Manyara anayedai kutapeliwa Sh1.7 milioni.

Shanzima amesema aliingia kwenye Kampuni ya Kalyanda miezi miwili hadi inakuja kufungwa aliwekeza mtaji wa Sh1.7 Milioni.

Amesema katika kiwango hicho alichowekeza alifanikiwa kuchukua Sh50, 000 huku akieleza kaka yake anayeishi Moshi ndiye aliyemshawishi kujiunga na alianza na kianzio cha Sh10, 000.

Shazima ambaye ni mfanyabiashara wa dagaa amekiri kuingia kwenye mtego huo ambapo aliamua  kuacha kazi yake na kuingiza mtaji wake wote kwenye kampuni hiyo ili anufaike zaidi.

Amesema wakati anaanza ndani ya mwezi wa kwanza aliona maendeleo mazuri kwa siku akijiingizia kiasi cha Sh80,000 lakini baada ya kuona biashara yake ya dagaa inayumba alicha na kuingiza fedha yote katika kampuni hiyo.

Naye Zacharia Joseph Mwanafunzi wa udaktari kutoka chuo cha Kampala anasema ameathirika kwa sababu walivyokuja walikuwa wanadai wanafanya uwekezaji kwa njia ya mtandao.

“Tuliingia kwa sababu ya uaminifu waliotupatia na vikao tulivyokuwa tunafanya nao na viongozi na mameneja wao tuliona wako makini na shughuli hiyo,”amesema

Amesema katika timu yake alikuwa watu 100 ikiwemo wahadhiri wawili na kati ya hao watano walikuwa wameweka kiwango cha Sh1 milioni huku mwenyewe akiweka Sh2.5milioni.

Amesema mtandao huo ulikuwa na zaidi ya Watanzania 10,000 na walichofanyiwa hawatakuja kusahau huku wakiiomba Serikali kuchukua hatua kali kuwasaidi warudishiwe fedha zao.