Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Boti yazama Indonesia, watu 166 wapotea

Muktasari:

Boti hiyo iliyoundwa kwa mbao haikuwa na orodha ya abiria waliokuwa wakisafiri, kwa hiyo maofisa wanategemea ripoti za familia za watu wanaosadikiwa kupotea ili kujua idadi ya abiria.


Jakarta, Indonesia. Watu wapatao 166 wanaaminika kwamba wamepotea baada ya boti iliyokuwa imewabeba kuzama katika Ziwa Toba Jimbo la Sumatra Kaskazini, maofisa wa Indonesia walisema Jumatano.

Boti hiyo ilizama Jumatatu mchana baada ya kuzidiwa kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa iliyosababisha mawimbi ya maji ya urefu wa mita mbili juu.

Boti hiyo iliyoundwa kwa mbao haikuwa na orodha ya abiria waliokuwa wakisafiri, kwa hiyo maofisa wanategemea ripoti za familia za watu wanaosadikiwa kupotea ili kujua idadi ya wanaoaminika kuwa waliwa abiri boti hiyo inayodaiwa ilikuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.

Mkuu wa kitengo cha majanga, Mahler Tamba, aliliambia shirika la habari la DPA kwamba kazi ya kusaka na kuokoa manusura ilikuwa inaendelea na hadi Jumatano asubuhi miili ya watu wawili waliokufa iliopolewa.

Mapema watu wanane waliokolewa na timu ya watu 350 inayofanya kazi hiyo.

Mahler alisema watu 166 walioorodheshwa kwamba wamepotea ni kwa mujibu wa ripoti za familia katika mji wa Tigaras wilaya ya Simalungun ambako boti hiyo ilikuwa inakwenda na Simanindo ambako walitoka.