Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BoT yataja sababu mbili kushuka shilingi

Muktasari:

Ripoti ya soko la fedha ya ya benki hiyo pia imeonyesha kuwa Dola ilikuwa ikibadilishwa kwa wastani wa Sh2,294 kama ilivyorekodiwa Ijumaa wiki iliyopita, kutoka Sh2,249 iliyobadilishwa Januari 29, mwaka uliopita.


Dar es Salaam. Benki Kuu (BoT), imesema kutokuwapo kwa bidhaa za kuuzwa nje ya nchi na pia watalii kupungua katika kipindi cha Januari zinaweza kuwa sababu za kushuka kwa shilingi dhidi ya Dola ya Marekani.

Mkurugenzi wa Uchumi, Utafiti na Sera wa BoT, Suleiman Misango alisema katika mahojiano na gazeti la The Citizen juzi kuwa katika kipindi cha miezi ya Desemba na Januari, shilingi ina kawaida ya kushuka na kupanda kulingana na Dola.

Kiwango cha ubadilishaji fedha za kigeni cha BoT kimeonyesha kuwa hadi juzi mauzo ya shilingi ya Tanzania yalikuwa Sh2,294 na ilinunuliwa kwa Sh2,271 ikilinganishwa na Sh2,249 na Sh2,227 iliyorekodiwa Januari 29, mwaka jana.

Ripoti ya soko la fedha ya ya benki hiyo pia imeonyesha kuwa Dola ilikuwa ikibadilishwa kwa wastani wa Sh2,294 kama ilivyorekodiwa Ijumaa wiki iliyopita, kutoka Sh2,249 iliyobadilishwa Januari 29, mwaka uliopita.

Hata hivyo, Misango alisema kuwa anguko hilo la shilingi linasababishwa na mwezi wa Januari kutokuwa po kwa bidhaa za kuuza nje ya nchi na pia wingi wa watalii.

“Kwa kawaida katika kipindi cha Desemba huwa inapanda lakini ikifika Januari kunakuwa na mahitaji makubwa kwa kuwa mashirika na watu binafsi wanazitafuta ili kukidhi mahitaji yao yanayohusu mwisho wa mwaka,” alisema.

Misango alisema mambo yatakuja kubadilika baada ya watalii kuanza kuongezeka nchini na uuzwaji wa bidhaa za ndani nje ya nchi, na hivyo wataongeza fedha za kigeni.

Juzi, maduka ya fedha yalikuwa yakiuza Dola moja kwa Sh2,385 ikiwa ni ongezeko kutoka Sh2,256 iliyorekodiwa Januari, 2018.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanasema kushuka huko kwa shilingi kunasababishwa na sababu za ndani na za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa Dola kuliko sarafu nyingine kubwa duniani.

Vilevile wanalitaja ongezeko la ununuzi wa bidhaa kutoka nje ya nchi kunakozidi mapato ya uuzwaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi yanayoingiza fedha za kigeni.

Hata hivyo, mmoja wa wachambuzi amelihusisha anguko hilo na kukwama kwa soko la korosho kuuzwa nje ya nchi, akisema kutouzwa huko pia kumeipotezea nchi fedha za kigeni hadi mwisho wa mwaka jana kwa kuwa hakukuwa na malipo yaliyofanywa.

Mwaka jana Serikali ilikusanya Dola 575 milioni za Marekani (sawa na (Sh1.3 trilioni) katika mauzo ya korosho nje ya nchi, jambo lililosaidia kuiimarisha shilingi dhidi ya Dola na fedha zingine za kigeni.