Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bodaboda waletewa vilainishi maalumu

Muktasari:

  • GSM imekuja na bidhaa mpya ya kilainishi kwa vyombo vya moto vya pikipiki na bajaji vinavyokuja kuboresha ufanisi wa injini na kuifanya idumu kwa muda mrefu na kutekeleza majukumu yao kwa uwakika zaidi.

Dar es Salaam. Katika kuendelea kulinda uimara na kuongeza ufanisi wa chombo cha usafiri, Kampuni ya GSM Spareparts imekuja na bidhaa mpya ya kilainishi cha injini za vyombo vya moto vya pikipiki na bajaji.

Kilainishi hicho kiitwacho 'Gsm speedy 4T' kinauwezo wa kutumika zaidi ya siku 14, kwa msingi huo kinakuja kuleta suluhisho kwa wamiliki vya vyombo hivyo waliokuwa wanalalamika injini za vyombo vyao vinakufa mapema kwa kukosa vilainishi bora.

Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Rukia Yazid amesema sifa kubwa ya kilainishi hicho ni kuboresha ufanisi wa injini na kuifanya idumu kwa muda mrefu.

"Kuwa na injini imara inayotumia kilainishi bora ni kuifanya safari ya chombo chako kisiwe salama na kisikumbwe na misuko suko huwapo barabarani na kuwafanya wafike mapema na tunajua wanatumia vyombo hivyo kibiashara," amesema Rukia.

Amesema kampuni hiyo ambayo ni wasambazaji wa vipuri vya vyombo vya moto nchini kama malori ya Kichina na betri za magari imesisitiza bidhaa hiyo itafikishwa maeneo yote nchini.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo kutoka kampuni hiyo, Yohana Bute amesema katika kufikia azma hiyo wataanzisha kliniki ya itakayowahusisha wataalamu kuwafikia watumiaji wa vyombo hivyo na kuwapa elimu.

“Tutazunguka kwenye vijiwe vyao na kutoa elimu lengo kuondoa changamoto changamoto na waanze kutumia kilainishi bora kitakachokuwa kinatunza injini zao na kuwahakikisha usalama muda wote,”amesema

Bute amesema katika Kliniki hizo watakuwa wanabadilishana ujuzi mambo ya kufanya kutunza Injini zao hasa katika kutumia kilainishi hicho katika kutunza vyombo vyao vya moto.

“Lengo letu ni kuwasaidia watanzania waboreshe maisha yao kwa kuwaletea bidhaa bora lakini zinapatikana kwa gharama nafuu na ikitumiwa itakuwa chachu ya kulinda chombo chake kwa muda mrefu,”amesema

Bute amesema wameanza na vilainishi vya Pikipiki na Bajaji lakini baadaye watakuja na vilainishi vya vyombo vingine huku akieleza bado wanaendelea kufanya utafiti kujua mahitaji halisi na uwekezaji.

“Hatutaki kufanya vitu vitakavyokuja kuleta changamoto lengo letu ni kukuza teknolojia,”amesema Bute.