Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bei ya petroli yashuka, dizeli yapaa

Muktasari:

 Bei za rejareja za mafuta ya Petrol kwa jiji la Dar es Salaam imepungua huku mikoa ya Tanga na Mtwara ikongezeka, Dizeli juu.

Dar es Salaam. Wakati bei za mafuta ya rejareja ya petroli yanayoingia kupitia Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zikipungua kwa viwango tofauti bei ya dizeli imepaa.

 Licha ya kupungua kwa bei ya petroli yanayopitia bandari hizo, wakazi wa mikoa ya Tanga na Mtwara watalazimika kuongeza fedha zaidi watakapohitaji huduma kutokana na bei kupaa hilo likichangiwa na bei iliyokuwapo mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), petroli inayopitia bandari ya Dar es Salaam imepungua kwa Sh59 huku ruzuku ya mafuta inayotolewa na Serikali katika eneo hilo ikiondolewa kwa mafuta ya Dar es Salaam.


Pia, bei ya petroli inayopitia Mtwara imepungua kwa Sh92 katika mwezi Desemba huku upande wa Tanga ikiongezeka kwa Sh9.

Hiyo ikiwa na maana sasa bei ya mafuta ya petroli kwa upande wa Dar es Salaam imeshuka hadi kufikia Sh2, 827 kutoka Sh2,886 iliyokuwapo Novemba mwaka huu.


Lakini kulingana na ukomo wa bei ya mafuta iliyokuwapo Novemba mwaka huu, bei ya petroli kwa upande wa Tanga imefikia Sh2,815 kutoka Sh2,806 na Mtwara wakinunua lita moja ya petrol kwa Sh2,825 kutoka Sh2,917.

Katika upande mwingine, bei ya dizeli ya rejareja kwa upande wa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara imeongezeka kwa Sh278, Sh422 na Sh416.

Kwa mujibu wa taarifa, ili kukabiliana na athari za ongezeko la bei za mafuta nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinatumia dizeli, Serikali imetoa ruzuku kwa bei ya Desemba 2022.

“Kutokana na ruzuku hiyo, bei ya mafuta ya dizeli imepungua kwa Sh83 kwa lita, Sh247 na Sh243 kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Dizeli sasa itauzwa kwa Sh3,247 kutoka Sh3,052 ilikuwapo Novemba mwaka huu kwa upande wa Dar es Salaam huku wakazi wa Tanga wakinunua Dizeli kwa Sh3,496 kutoka Sh3,249 na Mtwara kwa Sh3,512 kutoka Sh3,269