Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bashungwa atahadharisha wanaowania Jimbo la Kyela

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akisalimia wananchi (hawapo pichani) alipokuwa akikagua mradi wa barabara ya Ibanda -Kajunjumele yenye urefu wa kilometa 22. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema leo Jumatatu, Oktoba 2, 2023 wakati akizungumza na wanachama zaidi ya 1,000 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kyela akiwa ameambatana na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

Kyela. Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameonya watu walioanza kutangaza nia ya  kuwania nafasi mbalimbali za uongozi  katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na Mkuu wa 2025 kuwa wapime kina cha maji na hali ya mfuko.

 Bashungwa amesema leo Jumatatu Oktoba 2, 2023 wakati akiongea na wanachama wa CCM  zaidi ya 1,000, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya na kuweka wazi dhamira ya Serikali ni kuongeza nguvu kwenye miradi ya maendeleo nchini kwa wabunge walioaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tunaona kazi anazofanya mbunge wenu na ninyi wana CCM ndiyo wenye duka tembeeni kifua mbele kwani Mbunge mliyempa kura hamkupoteza tunamuelewa katika kutetea maslai ya wana Kyela,” amesema.


Bashungwa amewataka wananchi na wanachama wa CCM kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Kyela Ally Mlaghila kuhakikisha mwakani katika nafasi za Serikali za mitaa kuchagua viongozi wanaofaa kukiongoza chama na si wababishaji,” amesema.

Bashungwa amewaonya wanaowania nafasi hizo wapime uzito wa mifuko yao kwani Rais Samia Suluhu Hassan amemuamini Mbunge wa Jimbo la Kyela, Ally Mlaghila  na  ndiyo sababu ya kuletwa kwa miradi ya elimu, afya, barabara na maji kwa wananchi.

“Jamani mnaotangaza nia msikurupu kujinasibu kugombea jimbo la Kyela au majimbo mengine ya Mkoa wa Mbeya kama chama hatuko tayari kuwapoteza, huku akisisitiza wanaCCM kuwa macho kwenye  uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wakatekeleze ilani kwa kupiga kura za kishindo kuanzia kwenye ngazi za mashina,”amesema.

Aidha katika hatua Bashungwa amesema lengo la ziara yao na Waziri wa Fedha ni kukagua miradi ya barabara, ambayo Serikali ilitoa fedha katika Wilaya ya Rungwe na Kyela.

Naye Katibu Mwenezi CCM, Mkoa Bashiru Madodi amesema kwa sasa hakuna Jimbo litakalopotezwa kwani tayari safu katika majimbo yote zinajitosheleza.

Mbunge wa Kyela, Ally Mlaghila, amewaeleza wananchi kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya miradi ya maendeleo hususan elimu, afya barabara.

“Ndugu zangu wana Kyela mengi nimezungumza na kuomba kwa Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan na ndiyo mnaona ujio huu wa mawaziri wawili kutembelea miradi na kuona changamoto za wanakyela,” amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kuwa katika kutekeleza ilani ya uchaguzi Serikali imetoa zaidi ya Sh750 milioni kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela sambamba na Sh450 milioni ununuzi wa vifaa tiba.

Waziri Nchemba amesema kuwa mkataba mbunge na wananchi ni kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwataka wananchi kuwakataa wapinga maendeleo.

Amesema kuwa umefika wakati wa kuacha wananchi kukubali kudaganywa na badala yake kuunga mkono ili Serikali iendelee kukuza uchumi na kusogeza maendeleo ya nchi.

“Kwa kuwa kazi kubwa inafanyika na Serikali wananchi hampaswi kuwa wanyonge mtambue sasa tunaenda kwenye uchaguzi kuweni makini msicheze nyimbo za wengine wanaodandia kila ajenda  wanaCCM shikamaneni na kujua kuna watu wanatafuta ajenda za uchaguzi,”amesema.

Amesema umefika wakati wa kufanya siasa za kistaarabu na siyo kuleta vurugu, chuki matusi na dharau na kwamba  washindane na ilani za uchaguzi.