Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bakwata yatangaza Eid El-Adh'haa Juni 7, kuswaliwa kitaifa Dar

Muktasari:

  • Waislamu watakiwa kujiandaa vyema kwa ajili ya siku hiyo ambapo swala ya kitaifa na baraza la Eid vitafanyika jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) limetangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Adh'haa itakuwa Juni 7, 2025 na itaadhimishwa kitaifa jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Alhaj Nuhu Mruma imeeleza kuwa sherehe hiyo itaambatana na swala ya Eid itakayofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Alhaj Mruma swala hiyo itakayoanza saa 1:30 asubuhi ikimalizika litafuata Baraza la Eid.

“Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir anawatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya Sikukuu hii” imeeleza taarifa hiyo.

Eid El-Adh'ha ni sikukuu ambayo huadhimishwa baada ya Waislamu kukamilisha ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya mwisho katika nguzo tano za Uislamu.

  Hijja ni moja ya nguzo tano za Uislamu, ambazo zinaunda misingi ya imani ya Mwislamu. Kila Mwislamu anatarajiwa kuhiji angalau mara moja katika maisha yake ikiwa ana uwezo .

Tofauti na Swala, Sadaka na Saumu, Hijja inatakikana kwa kila Mwislamu mara moja tu katika maisha yake, ilimradi awe anastahiki kimwili, kihisia na kifedha. Hata hivyo, Waislamu wanaruhusiwa kwenda zaidi ya mara moja ikiwa wana uwezo.

Katika ibada ya Hijja, Waislamu hukusanyika kutoka pande zote za dunia wakitofautiana kwa mazingira yao, lugha, jinsia na rangi, wakielekea mahali pamoja, yaani uwanja wa Arafa.

Katika siku hiyo, hawamiliki chochote cha dunia isipokuwa mavazi ya kufunika miili yao.

Hufika Arafa wakiwa wamechafuka kwa vumbi na nywele timtim, wakiwa wameacha mali, watoto, vyeo na mamlaka yao kwa hiari, kwa lengo la kutekeleza ibada hii tukufu na kutafuta msamaha wa Allah Mtukufu.