Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba aliyekuwa akibaka watoto wake wawili kufia jela, afungwa maisha



Mwanza. Kuna methali ya Kiswahili inayosema siku ya kufa nyani miti yote huteleza, hii ndio imemkuta baba wa watoto wanne mkazi mkoani Geita kushindwa kujinasua na kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka wanawe wawili.

Mmoja wa watoto hao ana umri wa miaka 13 na alikuwa akiishi naye kama baba mlezi na mwingine mwenye umri wa miaka tisa ni mtoto wake wa damu (bilogical father), na alikuwa akiingia chumbani humo na kuwabaka.

Kosa la kwanza ni kuwabaka  (incest by male) ambalo ni la kuzini na maharimu kinyume na kifungu 158(1)(a) cha Kanuni ya Adhabu na kosa la pili ni la kubaka kinyume na kifungu 130(2(e) na 131 cha Kanuni ya Adhabu.

Kwa mara ya kwanza baba huyo ambaye jina lake tunalihifadhi ili kuwalinda watoto wake, alitiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Bukombe na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kosa la kwanza na kifungo cha maisha kwa kosa la pili.

Hakuridhika na hukumu na adhabu aliyopewa, akaamua kukata Rufaa Mahakama Kuu, kanda ya Mwanza ambapo rufaa yake ilitupwa, akakata rufaa Mahakama ya Rufani Tanzania, ambapo jopo la majaji watatu limeitupa rufaa hiyo.

Uamuzi wa kubariki adhabu hizo ulitolewa Julai 23,2026 na majaji Dk Mary Levira, Gerson Mdemu na Jaji Issa na kuwekwa katika tovuti ya TanzLII Julai 25,2026, ambayo ni tovuti rasmi ya Mahakama ya Tanzania.

Tukio la ubakaji lilivyokuwa

Kulingana na ushahidi wa shahidi namba moja na tatu wa upande wa Jamhuri, ambao ndio waathirika wa ubakaji huo, baba yao alikuwa anawafanyia ufedhuli huo kwa tarehe tofauti tofauti nyakati za usiku kati ya Desemba 2021 na Januari 2022.

Watoto hao walikuwa wakiishi na ndugu zao wengine wawili, mmoja akiwa na miaka mitano, mshitakiwa pamoja na mama wa kambo aliyekuwa shahidi namba sita.

Mama yao huyo wa kambo alikuwa akiwaacha watoto hao peke yao nyumbani na kwenda mjini anakojishughulisha na uuzaji wa pombe, hivyo mshitakiwa hutumia mwanya huo kuingia chumbani na kuwabaka watoto hao wawili.

Baada ya kuchoshwa na vitendo vya baba yao, mmoja wa watoto hao aliyekuwa shahidi namba tatu aliamua kumweleza mwalimu wake katika Shule ya Msingi Butambala ambako watoto hao walikuwa wakisoma darasa la sita na la tano.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, shahidi namba tano,Neema Samwel ambaye ni mwalimu wa shule hiyo, aliwasiliana na mama wa kambo wa watoto na kumtaka afuatilie suala hilo na akaahidi kufanya hivyo na atawalinda watoto hao.

 Mei 2022, suala hilo likaibuka tena ambapo watoto hao walirudi kuomba msaada kwa shahidi namba tano ambapo shahidi huyo aliitisha kikao kikimhusisha pia mshitakiwa ambaye alikiri kufanya vitendo hivyo na kuomba msamaha.

Mshitakiwa akaonywa asirudie tena kufanya kosa hilo, lakini siku tatu baadaye, watoto hao walitoa taarifa tena kwa mwalimu wao wakidai baba yao amewafuata tena na kutaka kuwabaka, na hapo mwalimu akaamua kutoa taarifa hiyo polisi.

Mshitakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani na watoto hao walipelekwa hospitali ambapo Ofisa Tabibu, Yohana Fumbuka ambaye ni shahidi namba saba aliwachunguza na kuthibitisha kuwa walikuwa wameingiliwa.

Kutokana na ushahidi wa watoto hao na mashahidi wengine wa Jamhuri na uzito wa ushahidi, ilimtia hatiani mshitakiwa na kumhukumu kifungo cha miaka 20 kwa ubakaji na kifungo cha maisha jela kwa kumwingilia mwanaye wa kumzaa.

Hakuridhika na hukumu hiyo, akafungua rufaa namba 143 ya 2022 katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ambapo ilitupwa Oktoba 18,2023 na kuamua kukata rufaa Mahakama ya Rufani ambayo nayo ilibariki adhabu aliyopewa.


Alivyogonga mwamba

Katika rufaa yake Mahakama ya Rufani, baba huyo aliegemea sababu 11 za Rufaa ikiwamo kwamba shahidi namba sita ambaye ni mkewe, hakujulishwa juu ya kifungu namba 130(1) cha sheria ya ushahidi na mahakama haikufafanua juu ya adhabu.

Lakini alienda mbali na kusema maelezo yake ya kukiri kosa yalipolewa na mahakama kinyume cha sheria na kwamba maelezo hayo hayakukidhi sifa ya kuwa kielelezo na mahakama ilikosea kuegemea katika maelezo hayo.

Pia akadai ushahidi wa upande wa utetezi haukutiliwa maanani, adhabu aliyopewa haikuelezwa katika hukumu, shitaka halikuthibitishwa bila kuacha mashaka, hati ya mashitaka ilikuwa na dosari na hakutambuliwa kikamilifu kisheria.


Hukumu ya Majaji

Katika hukumu yao, majaji waliosikiliza rufaa hiyo walipangua sababu moja baada ya nyingine na kueleza kuwa kwa uchambuzi wa ushahidi uliofanywa na mahakama za chini, wameridhika kuwa baba huyo alistahili adhabu aliyopewa.

Kuhusu madai yake kuwa hakutambuliwa katika eneo la tukio kwa kuwa mwanga haukuwa unatosheleza, majaji hao walisema watoto walitoa ushahidi kuwa taa zilikuwa zinawaka wakati anaingia chumbani kwao na walimtambua kikamilifu.

Wakinukuu ushahidi wa shahidi namba moja, unaeleza “mshitakiwa alikuwa anakuja amevalia kitenge na sweta na kila anapoingia ndio anazima simu, anavua nguo halafu anatuingizia dudu kwangu na kisha kwa shahidi namba tatu.”

Majaji walisema ushahidi huo unawaacha wasiwe na mashaka na ushahidi huo kwa kuwa kwanza huyo ni baba yao wanayemfahamu vizuri, matukio yalikuwa ni mengi, walieleza alikuwa anavaa nguo na alitumia muda mrefu chumbani.

Kuhusu mkewe ambaye ni shahidi namba sita kutoonywa kulingana na kifungu namba 130 cha sheria ya ushahidi, majaji walisema mahakama ingefanya hivyo kama mkewe huyo angekuwa hataki kutoa ushahidi dhidi ya mumewe.

Mbali na hoja hiyo, kuhusu hoja mahakama haikutoa adhabu yoyote kulingana na kifungu 312(2) cha CPA, wakili wa Serikali, Happiness Mayunga alikiri juu ya jambo hilo lakini akasema lilirekebishwa katika mahakama ya kwanza ya rufaa.

Majaji hao walisema baada ya kupitia mwenendo wa shauri hilo, wanashindwa kukubaliana na malalamiko ya mrufani kwani katika ukurasa wa 71 na 72 wa hukumu ya mahakama ya Rufani inaonyesha adhabu hiyo iliandikwa.

Kuhusu maelezo yake ya onyo, majaji walisema baada ya kupitia kumbukumbu wamebaini kuwa maelezo hayo hayako wazi ni lini mrufani alikamatwa jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria hivyo maelezo hayo yanafutwa katika rekodi.

Hata hivyo, walisema Ofisa aliyerekodi maelezo hayo ambayo yalipokelewa kama kielelezo PE3, alitoa ushahidi kuwa alimkuta mshitakiwa akiwa amekamatwa saa 1 usiku wa kuamkia Mei 27,2022, lakini una mashaka kwa kuwa siye aliyemkamata.

Pamoja na kufuta maelezo hayo, majaji hao walisema ushahidi unaobakia unajitosheleza kumtia hatiani mshitakiwa hivyo hawana sababu ya kubadili hukumu na adhabu aliyopewa na hivyo mahakama inabariki adhabu aliyopewa.