Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Sangu: Ufisadi, dhuluma ni matendo ya giza

Askofu wa Jimbo katoliki la Shinyanga, Liberatus Sangu 

Muktasari:

  • Wakristo wanasherekea sikukuu ya kufufuka Bwana Yesu Kristo ikiwa ni kuhitimisha siku 40 za mfungo wa Kwaresima.

Shinyanga. Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Liberatus Sangu amewataka waumini wa dini ya Kikristo kusherehekea Pasaka kwa matendo yenye nuru sio giza ili waweze kufufuka na Yesu Kristo.

Akizungumza kwenye misa ya mkesha wa Pasaka jana Jumamosi, Aprili 19, 2025  iliyofanyika Parokia ya Mama Mwenye Huruma iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga amesema:

"Kifo na ufufuko wa Yesu Kristo ni njia ya uzima kuelekea nchi ya ahadi, hivyo basi nawasihi kusherehekea siku hii kwa matendo ya mwanga, kutenda haki na siyo matendo ya giza kama ufisadi, dhuluma, unyanyasaji na matendo ya nuru hutimizwa na upendo pekee," amesema Askofu Sangu.

Pia amesema: "Kupitia ubatizo mwanadamu anauvua utu wa kale na kuuvaa utu mpya kwa kuondolewa dhambi ya asili na kufanya maandalizi ya kuelekea nchi ya ahadi," amesema Askofu Sangu.

Mmoja wa wazazi wa watoto waliobatizwa, Neema Jonathan amesema kupitia ubatizo wa mtoto wake sasa ametambulika kama Mkristo kamili.


"Kupitia ubatizo huu mwanangu katambulika kama Mkristo kamili na katika sherehe ya Pasaka nitakuwa balozi wa kwanza kusimamia watoto katika kufanya matendo ya mwanga katika siku zote," amesema Neema.

Naye muumini, Paschal Makere amesema moja ya matendo ya mwanga ni kushiriki Pasaka hiyo na wahitaji kwa njia hiyo tunashiriki ufufuko wa Yesu Kristo kikamilifu.

"Njia nzuri kusherehekea ni kuwatia moyo wafungwa, kwa chochote Mungu alichotupatia tugawane na wahitaji, namna watakavyo furahi ndivyo baraka zinavyoongezeka," amesema Makere.

Aidha, Askofu Sangu amewaomba wazazi kuwa wasimamizi na walinzi kwa watoto wao hasa katika matembezi ili kuwaepusha na majanga ya barabarani na  washerehekee kwa kiasi.