Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anayetuhumiwa kumuua mwanaye kupimwa akili

Mama aliyejulikana kwa jina la Johari (19) (mwenye Sweta) mkazi wa Mawelewele, Manispaa ya Iringa akiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kumuua mwanaye kwa kumzamisha kwenye ndoo ya maji ya chooni. 

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi mkoani Iringa limesema mama anayetuhumiwa kumuua mtoto wake kwa kumzamisha kwenye ndoo ya maji chooni atapimwa afya ya akili.

Iringa. Jeshi la Polisi mkoani Iringa, limeanza kumchunguza Johari Mbuma (19), mkazi wa Mawelewele, Manispaa ya Iringa, anayetuhumiwa kumuua mwanaye kwa kumzamisha kwenye ndoo ya maji chooni, ikiwamo kumpima afya ya akili.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema hayo leo Novemba 22, 2023, kwamba Johari anatuhumiwa kumuua mwanaye  Naifath Abdalah aliyekuwa na miezi saba.

"Huyu binti baba yake yuko Dar es Salaam amesema anataka kwenda huko kuhangaika akidai huku ni magumu yamemshinda, kwa hiyo katika safari yake ya Dar es Salaam baba yake alimwambia aende bila mtoto.

“Hivyo siku ya tukio alimbeba mtoto mgongoni na alienda naye chooni kujisaidia, akamtumbukiza kwenye ndoo ya maji,"amesema.

Awali Johari alisimulia kuwa alitoka kwao na kwenda kwa rafiki yake, lakini baadaye alipotataka kujisaidia, aliingia chooni ambako baada ya kumaliza shughuli zake alimtumbukiza mtoto kwenye ndoo nyeupe iliyokuwa na maji chooni humo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mawelewele, Obedi Mtatifikolo amesema alipata taarifa Jumapili, Novemba 19, 2021 kisha akachukua hatua ya kutoa taarifa polisi.

Mkurugenzi wa Shirika la Pamoja, John Paul amesema hatua ya kumpima akili kabla ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo imeonyesha uungwana na haki.

"Huenda alikamatwa na kifafa cha mimba au anayo shida ya akili akatekeleza mauaji hayo, suala la kumpima afya ya akili ndilo ambalo tulishauri zaidi," amesema Paul.