Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amuua mpenzi wake akimtuhumu kumuambukiza Ukimwi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo

Muktasari:

  • Wawili hao walikuwa wakiishi pamoja kama mke na mume kwa muda, kabla ya mtuhumiwa kuanza kumtuhumu Josephine ambaye kwa sasa ni marehemu kuwa ndiye aliyemwambukiza virusi vya Ukimwi, tuhuma zilizosababisha ugomvi ulioishia kwa mauaji.

Musoma. Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia Samwel Emmanuel (20) kwa tuhuma za mauaji ya Josephina Magani (52), kwa madai kwamba alimwambukiza virusi vya Ukimwi.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa baada ya Emmanuel kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo, alimlaumu Magani kuwa chanzo cha hali hiyo.

Inadaiwa kuwa kutokana na hasira hizo, alichukua hatua ya kumchoma Magani kwa kitu chenye ncha kali, na kusababisha kifo chake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, jana Alhamisi Mei 8, 2025, tukio hilo lilitokea Mei 7, 2025.

Amedai uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wawili hao walikuwa wakiishi kama mume na mke kabla ya mtuhumiwa kumtuhumu Magani kuwa chanzo cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Kamanda Lutumo amesema kuwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, Samwel aliburuza mwili wa marehemu na kuutumbukiza kwenye shimo lililotumika awali kuchimba dhahabu katika Kijiji cha Natta, wilayani Serengeti.

Amedai Magani alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kuchomwa tumboni kwa kitu chenye ncha kali.

“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi. Badala yake, watoe taarifa kwa vyombo husika ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria,” imeeleza sehemu ya taarifa ya Polisi.