Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amchinja mkewe akimtuhumu kuwa na mwanaume mwingine

Muktasari:

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia, Mapinduzi Siliya (45) kwa tuhuma za kumuua mkewe, Terezia Mtajiha.


Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia, Mapinduzi Siliya (45) kwa tuhuma za kumuua mkewe, Terezia Mtajiha.

Siliya anadaiwa kumchinja kwa kutumia kisu kisha mwili kuutupa mto Nzovwe jijini humo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano  Januari 11, 2022   na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu.

Kuzaga amesema kisa cha mauaji hayo ni mtuhumiwa kumtuhumu mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.

"Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine katika kubaini, kuzuia uhalifu ili kila mtu afanye shughuli zake katika hali ya amani," amesema Kuzaga.

Wilisi Kupasya jirani wa familia ya Siliya amesema wawili hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara hasa walipokuwa wanatoka kwenye starehe zao.