Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyenusurika kifo ajali ya moto Kariakoo afunguka

Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo Mnadani walioathiriwa na tukio la moto jana wakikusanya baadhi ya mabaki ya bidhaa zao na mabati yaliyokuwa yametenganisha vibanda hivyo kwaajili ya kuuza vyuma chakavu.

Dar es Salaam. Majeruhi moto wa Kariakoo Mnadani, ambao uliharibu majengo na kuteketeza mali na bidhaa za wafanyabiashara wa eneo hilo, amesimulia alivyonusurika kifo.

Akizungumza na Mwananchi Digital jana Alhamisi Oktoba 5, 2023, Mohamed Hamed amesema kuwa yeye na familia yake walikuwa wanajiandaa kwenda Zanzibar lakini ghafla aliitwa na mkewe na kuambiwa kuna moto.

"Mimi na familia yangu tulikuja kwenye harusi tukitokea Uingereza na harusi ilikuwa Ijumaa iliyopita baada ya hapo tukasema tupumzike nchini mwezi mmoja lakini janga la moto limetukuta tukiwa tunajiandaa kwenda Zanzibar," amesema.

Pia Hamed amesema kelele za mkewe zilimtoa ndani akiwa amevaa bukta na kukuta moshi ukiwa umetanda sebuleni na kuwaambia watoke nje na ghafla kukawa na giza.

"Wakati nawaambia watoke nje waliniambia hawaoni ndipo nilipowafuata na kuwaambia tutafute mlango lakini kutokana na giza tukajikuta tupo kwenye choo kilichopo usawa unapotokea moto," mesema Hamed.

Hamed amesema alipogundua kuwa walipoingia ni chooni si sehemu ya kutokea aliamua kuwashika mkono na kuwapeleka chumba kingine kwa kupapasa na ndipo waipopata majereha kutokana na joto la moto huo.

Kwa mujibu wa manusura huyo, mkewe amepata majeraha kwenye mikono na kwamba kwa sasa hawezi kufanya shughuli yoyote ikiwemo kujihudumia, huku mtoto wake akiwa amepata majeraha sehemu ya kifua kichwani na mgongoni.

"Wakati tunatafuta pa kutokea ndani kulikuwa na mvuke mkali ambao ulituunguza ikabidi tupige kelele ya kuhitaji msaada huku nikivunja mlango baada ya kufanikiwa kufika eneo la mlango," amesema na kuongeza kuwa "Nimeungua mikono na kuumia sehemu ya mguu kutokana na mvuke wa moto kuingia ndani wakati navunja vioo," amesema.

Amesema wakati wanatoka nje hakujua kama ameumia hadi pale alipoanguka na kupelekwa polisi kwa ajili ya kibali cha matibabu (PF 3).

"Nilipofanikiwa kutoka nje kwa kusaidiwa na watu wengine nilijikuta nashindwa kutembea kutokana na kubanwa na kufua na kushindwa kupumua huku damu zikiwa zinanitoka na nilibebwa na mtu wa bajaj baada ya kuanguka chini,” amesema na kuongeza;

“Baada ya kutoka polisi nilirudishwa tena eneo la tukio kwani mwenye bajaj hakujua wapi anipeleke na hapo tulikuta gari la wagonjwa nikaingizwa humo na kupelekwa Muhimbili nilipokaa siku nne," amesema.

Hamed amedai kuwa aliangalia usalama wa familia yake kwanza na hivyo aliamua kuwakinga na kila lililokuwa mbele yao huku yeye akijitoa mhanga wa kubaki nyuma na hata majeraha aliyoyapata yametokana na kupigania uhai wake na familia yake.

Awali Hamed amesema hakujua mtoto wake na mkewe wapo wapi kwani kila mmoja alichukuliwa na watu tofauti na walikutana kwenye huduma ya dharura hospitalini hapo.

Kuhusu moto kuanzia kwenye chumba chao amesema wao ni wageni na kwenye vyumba walivyopewa hakukuwa na jiko hivyo ni vigumu moto kuanzia kwao.

"Madai yanayotolewa kuwa moto umeanzia kwetu si kweli maana vyumba vyetu sisi havijaungua bali pamekuwa vumbi la moshi ambalo limechafua ukuta,"

Hata hivyo Hamed amesema amepoteza vitu vyake ikiwepo pochi yake ambayo ilikuwa na pesa pamoja na vitu vya mtoto wake.

Kutokana na ajali aliyoipata waliogopa kuendelea kulala kwenye hiyo nyumba na kuomba kutafutiwa sehemu nyingine jambo ambalo lilitimizwa na mwenye nyumba wao.

Ikumbukwe ajali hiyo ya moto iitokea eneo la Mnadani Kariakoo ambapo chanzo chake hakijajulikana na kusababisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kuunda kamati itakayochunguza tukio hilo.