Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekutwa akisafirisha bangi kilo 216 jela maisha

Muktasari:

  • Siku ya tukio katika Kijiji cha Lumba-Chini, mkoa wa Morogoro, Damas Makenza alikutwa akisafirisha dawa hizo za kulevya zilizokuwa na uzito wa kilo 216 ambapo mahakama baada ya kusikiliza hoja za pande zote imemkuta na hatia na kumuhukumu adhabu hiyo.

Arusha. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Masijala Ndogo ya Morogoro, imemuhukumu kifungo cha maisha, Damas Makenza baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi kilo 216.

Hukumu hiyo ilitolewa Juni 17, 2025 na Jaji Sedekia Kisanya aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi  ya mwaka 2024 na nakala yake kuwekwa kwenye mtandao wa Mahakama.

Damas alidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na (3) (iii) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya , Sura ya 95 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019 na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Kifungu hicho kilisomwa pamoja na aya ya 23 ya jedwali la kwanza la sheria na vifungu vya 57(1) na 60 (2) vya Sheria ya Kudhibiti Uhalifu wa Kiuchumi na Kuratibu (EOCCA).

Katika kesi hiyo ilielezwa mahakamani hapo kuwa Julai 26, 2023, katika kijiji cha Lumba-Chini, mkoa wa Morogoro, Damas alikutwa akisafirisha dawa hizo za kulevya kilo 216.

Jaji Kisanya baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, amesema Mahakama imemkuta Damas na hatia na kumuhukumu adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na mawakili watatu wakiongozwa na Monica Matwe ambao waliwasilisha mashahidi tisa na vielelezo 10.

Ilielezwa siku ya tukio wakati DCEA wanaendelea na operesheni yao mkoani humo, walipokea taarifa kuwa kuna biashara ya dawa za kulevya inafanyika usiku katika eneo hilo na uliwekwa mtego, kutokana na ugumu wa kulifikika eneo hilo, walilazimika kuacha magari yao na kupita kwa miguu katika msitu.

Shahidi wa nane, Inspekta Msaidizi, Lazaro Mhegele amesema walipokaribia eneo hilo, waliona watu wakikimbia  na walifanikiwa kumkamata Damas aliyekuwa na tochi akikagua mifuko saba, ambayo ilikuwa eneo hilo iliyokuwa na majani makavu yaliyoshukiwa kuwa dawa za kulevya aina ya bangi.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa sampuli za majani hayo zilipelekwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), na majibu yalionyesha kuwa ni bangi.


Utetezi

Akijitetea mahakamani hapo, Damas alidai kukamatwa Julai 25, 2025 akitokea kwenye mkutano wa kupanga mahafali ya Shule ya Msingi Singisa.

Alieleza kuwa baada ya kukamatwa, alipelekwa katika eneo ambalo tayari maofisa wengine wa polisi walikuwa wamekusanyika na watu wengine watatu pia walifikishwa eneo hilo na wakawekwa pamoja. Aliongeza kuwa alipoomba ruhusa ya kuwasiliana na kiongozi wa kijiji, ombi lake lilikataliwa.

Aidha, alikana kumiliki mifuko hiyo iliyokuwa na dawa hizo za kulevya na kwamba, hakuwahi kusaini cheti cha ukamataji kwa sababu hajui kusoma wala kuandika na akaiomba Mahakama imuachie huru kwa kuwa hana kosa.


Uamuzi Jaji

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Jaji Kisanya amesema Mahakama katika kufikia uamuzi wake itazingatia jumla ya ushahidi, pamoja na hoja za kisheria zilizotolewa katika mawasilisho ya mwisho.

Amesema miongoni mwa masuala Mahakama inayozingatia ni iwapo mifuko saba ya salfeti iliyokuwa na majani makavu ilikamatwa kwa Damas, kama upekuzi na ukamataji huo ulifanywa kihalali, kama mifuko hiyo ilikuwa na kilo 216 za bangi na iwapo mlolongo wa ulinzi ulitunzwa ipasavyo.

Jaji Kisanya amesema baada ya kuzingatia ushahidi wa pande zote mahakama inamkuta Damas na hatia ya kukutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi iliyokuwa na uzito wa kilo 216.

“Damas ametiwa hatiani chini ya kifungu cha 15(1)(a) na (3)(iii) cha Sheria ya Kudhibiti na Utekelezaji wa Dawa za Kulevya ,kama ilivyorekebishwa (DCEA),na masharti ya kifungu cha 60 (2) cha EOCCA ambayo inaeleza hukumu ya lazima ya kifungo cha maisha,”amesema