Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyebaka, kulawiti mtoto wa miaka sita akwaa kisiki Mahakama ya Rufani

Muktasari:

  • Mahakama ya Rufani imebariki kifungo cha maisha jela alichohukumiwa mkazi wa Kilwa, George Amiri, aliyohukumiwa kwa kulawiti na kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita.

Arusha. Mahakama ya Rufani imebariki adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa mkazi wa Kilwa, mkoani Lindi, George Amiri, aliyehukumiwa kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita.

Hii ni rufaa yake ya pili kukwaa kisiki, awali alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilwa baada ya kutiwa hatiani.

Alikata Rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara iliyogonga mwamba na kuridhia hukumu ya Mahakama ya awali.

Mahakama ya rufani imetupilia mbali rufaa baada ya kuona haina mashiko kwa kuwa, adhabu iliyotolewa ilikuwa sahihi.

Katika kesi ya msingi, Amiri alishitakiwa kwa makosa ya  ulawiti na ubakaji anayodaiwa kutenda kinyume na kifungu cha 154 (1) (a) na (2) pamoja na vifungu vya 130 (1) (2) (e) na 131 (1) vya Kanuni ya Adhabu.

Ilidaiwa Septemba 2, 2020 katika Kijiji cha Nakiu Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, alimlawiti na kumbaka mtoto wa kike wa miaka sita.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watatu na kielelezo kimoja.

Shahidi wa kwanza (mama wa mwathirika), alidai siku ya tukio saa sita mchana, mrufani ambaye ni mmoja wa majirani zake alifika nyumbani kwake akiwa na baisikeli, alimuomba amwitie mtoto wake ili akamnunulie pipi dukani.

Alidai kuwa alimjibu mrufani kuwa ampe mtoto hiyo hela ili akanunue lakini mrufani alidai anataka kwenda na mtoto huyo, pesa itakayobaki aondoke nayo.

Shahidi alidai alikubali na mrufani aliondoka na mwathirika huyo lakini hadi jioni mtoto huyo hakuwa amerudi nyumbani, ndipo walianza kupata wasiwasi kwa kuwa mrufani alikuwa mlevi, hivyo wakaanza kumtafuta katika duka alilodai kwenda na baa mbalimbali.

Alidai baadaye alienda kwa mama wa mrufani aliyemwambia kuwa, mrufani alikwenda kukusanya majani ya mitende kwa ajili ya kujenga paa la nyumba yao,  ndipo alipomjulisha mumewe juu ya kupotea kwa mtoto na kuripoti kwenye uongozi wa kata na kuanza kumtafuta mrufani.

Alidai kuwa baada ya upekuzi kuendelea kijijini hapo, wanakijiji walimkuta mtoto huyo kando ya Barabara ya Nanjilinji na baada ya kumuuliza anapotoka alidai ametoka kwa mrufani.

Ilidaiwa kuwa shangazi wa mtoto huyo alipomwangalia mtoto huyo alibaini amebakwa na kulawitiwa.

Akitoa ushahidi wake mahakamani hapo, mwathirika huyo alidai mrufani alimbeba kwenye baiskeli na walipofika katika barabarani hiyo alimvua nguo na kuingiza uume wake kwenye njia yake ya haja kubwa na sehemu zake za siri.

Alidai kuwa hakuweza kupiga kelele kwa kuwa mrufani alimtishia kwamba, akijaribu kupiga kelele, angemkata na wembe na baada ya kumfanyia vitendo hivyo alimuacha eneo hilo.

Daktari katika ripoti ya uchunguzi iliyotolewa mahakamani, alibainisha kuwa mwathirika huyo alikuwa na michubuko mingi sehemu zake za siri.

Mrufani alijitetea na kudai alikuwa anamfahamu shahidi wa pili na siku ya tukio, alipita nyumbani kwa shahidi huyo ambaye alimuomba Sh2,000 alizompatia na akakana kuhusika na tukio la ubakaji na ulawiti.

Alidai kuwa siku hiyo alikuwa akienda kuokota majani ya michikichi na wakati akirudi alizingirwa na kundi la watu waliomvamia na kumfikisha kwenye ofisi ya kata na kudaiwa kufanya makosa hayo.

Mahakama hiyo ya wilaya baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili ulimkuta mtuhumiwa huyo na hatia na kumhukumu kifungo cha maisha jela na kuamriwa kumlipa fidia ya Sh1 milioni mwathirika huyo.

Mahakama Kuu/Rufaa

Rufaa ya mrufani mbele ya Mahakama Kuu iligonga mwamba, kwa kuwa Mahakama ya kwanza ya rufaa ilitupilia mbali rufaa hiyo na kuridhia hukumu ya Mahakama hiyo.

Mrufani huyo hakukata tamaa, alikata rufaa Mahakama ya Rufani nchini huku akiwa na sababu saba ikiwamo kuwa kesi upande wa mashtaka haikuweza kuthibitishwa, mwathirika kulazimishwa nini cha kusema mahakamani na Mahakama kuegemea ushahidi wa mwathirika na utetezi wake kutozingatiwa.


Rufaa

Katika Mahakama ya rufani, mrufani huyo alijitetea mwenyewe huku upande wa mjibu rufaa ukiwakilishwa na Wakili Faraja George, ambaye aliieleza Mahakama kuwa hoja ya mrufani kuwa utetezi wake haukuzingatiwa siyo ya kweli.

Wakili George alieleza kuwa, Mahakama ya awali ilizingatia vya kutosha utetezi alioutoa mrufani huyo na kuukataa kwa kuwa haukuweza kudhoofisha ushahidi uliotolewa na upade wa mashtaka.

Kuhusu hoja ya makosa hayo kutothibitishwa, alisema yalithibitishwa bila kuacha shaka na kwamba, ushahidi wa mashahidi hao haukukinzana kama alivyodai mrufani.

Katika hoja za upande wa mjibu rufaa, mrufani hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kuiomba Mahakama izingatie sababu zake za kukata rufaa, iruhusu rufaa hiyo na kumwachia huru kwa kuwa alisema alikuwa gerezani kwa miaka minne.

Mahakama hiyo ya rufani iliyoketi Mtwara, ilikuwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Rehema Kerefu, Sam Rumanyika na Agness Mgeyekwa, ambao walisikiliza rufaa hiyo ya jinai namba 38 ya mwaka 2022.

Katika uamuzi wao uliosomwa Juni 11, 2024, walikataa hoja zote za rufaa na kueleza kuwa wameridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka uliothibitisha kesi hiyo bila shaka yoyote.

Walieleza kuwa,  baada ya kusoma rekodi wanakubaliana na wakili wa Serikali kwamba utetezi wa mrufani ulizingatiwa na kuhusu hoja kuwa kesi haikuthibitishwa kwa kiwango kinachotakiwa, haina mashiko.

Walieleza kuwa, kesi ilithibitishwa bila kuacha shaka kupitia ushahidi wa shahidi wa pili ulithiobitishwa na shahidi wa kwanza na wa tatu na hakukuwa na ukinzani katika ushahidi wao.

“Baada ya kutafakari kwa makini mawasilisho yaliyotolewa na wahusika kwa misingi hii na kukagua rekodi nzima ya rufaa, tunakubaliana na Wakili George kwamba Mahakama zote mbili zilizo chini zilitathimini ipasavyo ushahidi na ziliridhika kwamba kesi dhidi ya mrufani ilithibitishwa bila kucha shaka.

“Tumepitia tena ushahidi wa shahidi wa kwanza na pili, na hakuna shaka walielezea tukio hilo kwa uwazi hasa shahidi wa kwanza aliyeeleza namna mrufani alienda na baiskeli na kumchukua shahidi wa pili na kutoweka naye siku nzima.

“Shahidi wa pili pia alielezea jinsi mrufani alivyomlawiti na kumbaka, alionyesha wazi jinsi mrufani alivyomvua nguo na kuingiza uume kwenye uke na sehemu yake ya haja kubwa, huku akimtisha kuwa akipiga kelele atamkata na wembe,”yanaeleza maelezo ya majaji.

Jipo hilo la majaji lilieleza kuwa, katika kesi zinazohusu makosa ya kingono, ushahidi bora ni ule wa mwathiriwa huku wakinukuu mashauri mbalimbali na kueleza katika kesi hiyo ushahidi wa mwathirika ulithibitishwa pia na shahidi wa kwanza na tatu.

Kutokana na mazingira hayo, majaji hao walielea hawaoni sababu za kutofautiana na mahakama za chini na na kutupilia mbali rufaa hiyo.