Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Akutwa na kakakuona 650 kwenye jokofu

Muktasari:

Msemaji wa Jeshi la Polisi la Java, Raden Prabowo amesema walipata taarifa kutoka kwa majirani walioshtushwa na nyendo za mwenye nyumba hiyo ambaye alikuwa anamiliki majokofu zaidi ya kumi

Dar es Salaam. Polisi nchini Indonesia wamekamata kakakuona zaidi ya 650 waliokuwa wamehifadhiwa kwenye jokofu katika nyumba ya mwanaume mmoja, mkazi wa wilaya ya jombag, kisiwa cha Java.

Msemaji wa Jeshi la Polisi la Java, Raden Prabowo amesema walipata taarifa kutoka kwa majirani walioshtushwa na nyendo za mwenye nyumba hiyo ambaye alikuwa anamiliki majokofu zaidi ya kumi

Inaelezwa kuwa mwenye nyumba hiyo mwenye umri wa miaka 55(jina linahifadhiwa) alikuwa akiwahifadhi kakauona hao na kuwatumia kwa ajili ya tiba za jadi.

Kakakuona hao, ambao ni miongoni mwa wanyama walio hatarini kutoweka,  walikutwa wakiwa wamefungwa kwenye mifuko ya nailoni na kuwekwa kwenye majokofu makubwa.