Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Akutwa akiwa amefariki bafuni

Muktasari:

  • Mtu mmoja akutwa akiwa amefariki bafuni katika eneo la Libya Manispaa ya Mtwara Mikindani huku akiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha kali ubavu wa kushoto.

Mtwara. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia mtu mmoja huku likiwatafuta wengine wakituhumiwa na mauaji ya mtu mmoja mkazi wa Mtaa wa Libya Kata ya Ufukoni Manispaa ya Mtwara Mikindani aliyekutwa akiwa amechomwa na kitu chenye ncha kali ubavu wa kushoto bafuni kwake.

Akitoa taaarifa hiyo kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo alisema kuwa mtu huyo alikutwa akiwa na jeraha ubavu wa kushoto linalooonyesha kuwa alichomwa na kitu chenye ncha kali.

Amesema kuwa tukio hilo la mauaji limetokea Julai 15 majira ya usiku huko Libya Kata ya Ufukoni Wilaya ya Mtwara ambapo Ahmad Abdulahman (51) mkazi wa Libya alikutwa bafuni kwake akiwa amefariki dunia huku akiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha kali.

Aidha Kamanda huyo amesema kuwa uchunguzi wa mwili wa marehemu uliofanywa na daktari umebaini kuwa sababu ya kifo chake ni kuvuja kwa damu nyingi kutoka katika jeraha hilo katika ubavu wa kushoto.

Polisi wamesema tayari mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwaajili ya mazishi wakati uchunguzi wa tukio hilo bado ukiendelea na tayari mtuhumiwa mmoja amekamatwa kwa mahojiano zaidi.

“Nitoe rai kwa jamii yetu kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya mauaji,” amesema

Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote watakao bainika kujihusisha na uharibifu aina yoyote ambao ni kinyume cha sheria ya nchi.