Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali ya basi, gari dogo yaua watu watatu na kujeruhi Same

Muktasari:

  • Ajali hiyo imetokea ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu tukio jingine kubwa la ajali lililotokea Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same Mjini, watu 42 walifariki dunia.

Moshi. Watu watatu wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha gari dogo aina ya Toyota Land Cruiser na basi la Kampuni ya Tahmeed. Ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Tanga – Arusha, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Tukio hilo limetokea leo Jumapili, Aprili 26, 2026, saa sita usiku baada ya dereva wa gari dogo kudaiwa kupoteza mwelekeo na kuvuka upande wake wa barabara, kisha kugongana uso kwa uso na basi hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa akizungumza na Mwananchi Digital, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akieleza kuwa ilitokea saa sita usiku wa Aprili 26, 2026.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same, Alexander Alex amesema wamepokea miili ya watu watatu pamoja na majeruhi wanne katika Hospitali ya Mji Same.

Basi kampuni ya Tahmeed na gari aina ya Toyota Land Cruiser likiwalimepata ajali Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Dk Alex amesema majeruhi watatu wamefikishwa hospitalini usiku wa tukio, huku mmoja akifikishwa asubuhi na kufanya jumla ya majeruhi kuwa wanne.

Dk Alex ameongeza kuwa hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu, na wote wameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya afya zao kuimarika.

Toyota Land Cruiser likiwa limepata ajali Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu tukio jingine kubwa la ajali lililotokea Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same Mjini, watu 42 walifariki dunia.

Katika ajali hiyo, basi la Kampuni ya Chanel One lililokuwa likitoka Moshi kuelekea Tanga liligongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Toyota Coaster lililokuwa likitoka Same kwenda Moshi kwenye sherehe ya harusi, kabla ya magari hayo kuwaka moto.


Endelea kufuatilia Mwananchi Digital kwa taarifa zaidi.