Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahukumiwa miaka mitatu jela kwa wizi wa mbuzi

Mwita Karege mkazi wa kijiji cha Nyiboko akisindikizwa na askari baada ya kuhukumiwa ma Mahakama ya Wilaya ya Serengeti  kifungo cha miaka mitatu kufuatia kukiri kosa la kuiba mbuzi watatu. Picha na Anthony Mayunga.

Muktasari:

  • Hakimu mkazi wa wilaya ya Serengeti, Adelina Mzalifu amemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela, mkazi wa kijiji cha Nyiboko, kata ya Kisaka, Mwita Karege(19) baada ya kukiri kuiba mbuzi watatu wenye thamani ya Sh150,000.

Serengeti. Mkazi wa kijiji cha Nyiboko, kata ya Kisaka, Mwita Karege (19) amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukiri kuiba mbuzi watatu wenye thamani ya Sh150,000.

Hukumu hiyo katika kesi ya Jinai namba 326/2020 imesomwa leo Jumatatu Oktoba 25 na hakimu mkazi wa wilaya Adelina Mzalifu kufuatia mshitakiwa kukiri mahakamani hapo kuiba mbuzi hao.

Amesema kutokana na kosa alilotenda, mahakama inamhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo.

Awali, mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Paschal Nkenyenge ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 29, 2020.

Na kuwa alikutwa na mbuzi watatu wenye thamani ya Sh150,000, mali ya Mugusuhi Mwita, mkazi wa kijiji hicho, akidaiwa kuwapeleka mnadani kuuza.

Hata hivyo mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea alidai hana la kujitetea.