Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afariki dunia baada ya kugongwa gari, chanzo mwendokasi

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ,Janeth Magomi.

Muktasari:

  • Mkazi wa Kata ya Ibinzamata Magembe Shija (56) amefariki dunia baada ya kugongwa gari, dereva atafutwa

Shinyanga. Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linachunguza tukio la kugongwa na gari mkazi wa Mtaa wa Sido, Kata ya Ibinzamata Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Magembe Mabula Shija (56) na kufariki papo hapo kisha dereva wa gari hilo kukimbia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Aprili 08, 2025 Kamanda wa Jeshi la Polisi Shinyanga, Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea jana Aprili 07, 2025 saa mbili usiku.
“Saa mbili usiku tulipokea taarifa ya ajali iliyosababisha kifo cha mtu mmoja aliyekuwa akitembea kwa miguu, maeneo ya stendi kuu ya mabasi Ibinzamata, baada ya kugongwa na gari hiyo dereva pamoja alitoweka, Jeshi la Polisi linamfatilia dereva huyo,” amesema Magomi.

“Katika uchunguzi wa awali tumegundua kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hilo na kushindwa kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara,” amesema Magomi.

“Tunaendelea kusimamia taratibu na sheria za usalama barabarani na tutakuwa wakali kweli kweli kwa wasiofuata sheria za usalama barabarani na kuhusiana na kifo cha mtu huyo tunaendelea kufatilia ni nani aliyesababisha na hatua kali zitachukuliwa.”