Absa yazindua kampeni ya droo ya magari kwa wateja wake

Muktasari:
- Watumiaji wa benki ya Absa wametakiwa kufanya miamala kidigitali ili kujishindia gari kupitia kampeni ya kushinda ndinga kunaweza kubadili stori yako.
Dar es Salaam. Katika kufanikisha ndoto za Watanzania wengi nchini ya kumiliki magari, benki ya Absa imeahidi kuendelea kutoa mchango yake kwa jamii kwa kuandaa mashindano ya kinyang’anyiro hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10, 2024 Mkurugenzi wa Fedha, Bernard Tesha amesema wameamua kuishi katika maisha ya wateja wao pamoja na wale ambao bado hawajajiunga na kuona thamani yao.
“Kwa kutumia miamala ya kimtandao au kadi za ATM, wateja wanapata fursa ya kushinda zawadi nono ya magari matatu mapya aina ya Subaru Forester ya mwaka 2014, huku wakifurahia huduma bora na salama za kifedha,” amesema Tesha.
Tesha amesema kampeni hii inalenga kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kifedha miongoni mwa wateja wa Absa, hasa katika mazingira ambayo ulimwengu unazidi kuhamia kwenye huduma za kidigitali.
Mkuu wa kitengo cha wateja katika Absa, Ndabu Swere amesema kampeni hii ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa kutoa motisha kwa wateja wake na kuhimiza matumizi ya njia mbadala za kulipa, ambazo ni salama na rahisi na itadumu kwa miezi mitatu kuanzia Septemba hadi Desemba.
"Lengo letu ni kuwawezesha wateja kupata huduma za kifedha bila usumbufu na kwa usalama zaidi. Kampeni hii pia ni njia ya kushukuru kwa ushirikiano wao wa kudumu na benki yetu," amesema Swere.
Amesema ili kuingia kwenye droo ya kushinda gari kwa watumiaji wa online wanatakiwa kufanya miamala ya Sh3 milioni huku wale wanaotumia mashine za ATM wanatakiwa kufanya miamala ya Sh5 milioni.
“Hapa wanaweza kufikiria kuwa ni kuweka na kutoa tu hata kununua bidhaa kupitia online ikiwepo umeme, kulipia bili za maji na matumizi mengne unaingia moja kwa moja na unaweza jishindia gari kwa kiasi hicho,” amesema.
Mteja wa benki hiyo Alex Jonson amesema hiyo inakwenda kutimiza ndoto za watu ambao watabahatika kushinda licha ya uwepo wa kauli kuwa magari yanayyotolewa yanakuwa yana mshindi tayari.
“Binafsi nitakuwa nafasa miamala yangu kawaida kwa sabbau huwa napitiliza kiwango walichosema na ikitokea nimeshinda nitaweka ushuhuda wa kweli wa kushinda ndinga na kubadili stori yangu,” amesema Jonson.