Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Watafiti wapewe uhuru’

Muktasari:

  • Ili kuleta tija katika tafiti zinazofanyika nchini, watafiti na wanazuoni nchini wametaka kupewa uhuru wa kuwasilisha kazi zao kulingana na mahitimisho waliyopata bila kujali upande utakaopendezwa au kuchukizwa nayo.

Dar es Salaam. Wanazuoni na wahadhiri katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), wamesema ili kuwa na utafiti wenye tija kwa Taifa nchini, watafiti wanapaswa kuwa huru, hata kama matokeo yake yatawachukiza watunga sera.

Wamesema kumekuwa na tabia ya vyombo vya dola kuingilia utafiti hasa ule ambao hauwapendezi baadhi ya watu Serikalini.

Akizungumza mwishoni mwa wiki Dar es Salaam katika mjadala uliozungumzia ‘haki ya kitaalamu na wajibu wa wanataalamu Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siaasa na Utawala kwa Umma, Dk Ng’wanza Kamatta amesema kazi za ubunifu zinahitaji uhuru na mazingira ya uhuru wa kifikra.

Amesema watafiti wanapaswa kuwa na uwanja mpana wa kutafakari mambo bila kuwa na wasiwasi kwamba hitimisho la utafiti wao hautawapendeza baadhi ya watu.

“Watafiti wapewe uhuru na nafasi za kuzitumia akili zao kufanya tafiti zitakazoongoza mahitimisho ya yale waliyokuokutana nayo bila kujali kuna wanaochukizwa na mahitimisho hayo,” amesema

Amesema kwa nyakati mbalimbali kumekuwepo na mapambano ya kitaaluma baina ya watanataalamu na vyombo vya dola ndani ya vyuo vikuu hasa kunapofanyika tafiti zisizoleta taswira nzuri kwa watunga sera.

“Tangu chuo kimeanza kumekuwa na udhibiti wa mambo yanayotokea kwenye chuo hiyo inaminya uhuru wa kitaaluma, wanataaluma kwa kutaka uhuru huo wamekuwa katika nyakati za mapambano na dola inayoilingilia uhuru wao, wanadai uhuru wa kufanya utafiti wao bila kuingiliwa,” amesema.

Kwa upande wake Mwanazuoni Mkongwe nchini Profesa Issa Shivji, amesema hakuna haja ya watafiti kufanya tafiti na kuzipeleka kwa watunga sera badala yake wafanye utafiti wenye kugusa maisha ya wananchi. 

“Wakifanya utafiti utakaogusa maisha ya wananchi hakutakuwa na haja ya kupeleka utafiti kwa watunga sera, wananchi wenyewe watadai haki yao kwa kuwashurutisha kutelekeza yaliyobainishwa kwenye utafiti,” amesema.

Kwa upande wake Dk Richard Sambaiga kutoka Idara ya sosholojia ya chuo hicho, amesema, utamaduni wa kuchukua maoni ya wasomi nchini umepungua hivyo wasomi wanapaswa kuchukua nafasi ya kuwaeleza watunga sera yapi wanapaswa kufanya kulingana na tafiti wanazozifanya.

“Wabuni njia mbadala wawa kufikisha hayo maoni ya kisomi maoni mengine huwa hayapenelewi sana sasa tutafikishaje kwa watoa maamuzi ambao wanaona yaliyofanyika hayawapendezi,” amesema.