Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upelelezi kesi ya 'Dk Manguruwe' wapigwa kalenda

Mshtakiwa Simon Mkondya (aliyevaa kaunda suti) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Muktasari:

  • Mkondya na Rweyemamu wakabiliwa na mashitaka ya kuendesha upatu, kutakatisha fedha, matukio yanayodaiwa kuyatenda kati ya Januari Mosi, 2020 na Desemba Mosi, 2023 jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Upelelezi kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40), maarufu  Dk Manguruwe, haujakamilika.

Mkondya na mwenzake, Rweyemamu John (59), ambaye ni Mkaguzi wa fedha wa kampuni hiyo, wanakabiliwa na mashitaka 28 yakiwamo ya kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji fedha linalomkabili Mkondya pekee yake.

Hata hivyo, John ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, yupo nje kwa dhamana baada ya kwenda kuiomba Mahakama Kuu na pia hana mashitaka ya kutakatisha fedha.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Novemba 5, 2024 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi ya mwaka 2024.

Leo Mei 15, 2025, wakili wa Serikali, Winiwa Kasala ameieleza Mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Anna Magutu kuwa Serikali bado inaendelea na uchunguzi, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, kesi hiyo imesikilizwa kwa njia ya mtandao huku Mkondya akiwa gerezani na mshtakiwa wa pili ambaye yupo nje kwa dhamana alikuwepo mahakamani hapo.

Hakimu Magutu alikubaliana na upande wa mashitaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 29, 2025 kwa kutajwa.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, kati ya mashtaka hayo 28, mashtaka 19 ni ya kuendesha biashara ya upatu na tisa ni ya kutakatisha viwanja.

Inadaiwa kuwa Mkondya akiwa mkurugenzi wa kampuni hiyo na John akiwa  mkaguzi wake waliendesha  biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu watapata pesa mara mbili hadi  tatu kama faida zaidi ya waliyotoa.

Washtakiwa hao wanadaiwa kujipatia Sh92.2 milioni kutoka kwa watu 19 tofauti ambao walitoa kiasi tofauti cha fedha kwa kuwaahidi kuwa watapata faida mara mbili hadi tatu ya fedha walizotoa.