Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA yamwaga ajira 400

Muktasari:

  • Ajira mpya 400 ambazo TRA wametangaza ni pamoja na za wachambuzi biashara, maofisa forodha na maofisa kodi, yeyote mwenye sifa anaweza kutuma maombi kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza ajira 400 ikiwamo zile zinazohusu maofisa forodha, maofisa kodi na wachambuzi biashara.

Tangazo lililotolewa jana na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, limewataka Watanzania wenye sifa kutuma maombi yao kabla ya Julai 17 mwaka huu.

Nafasi nyingine zilizotangazwa ni zile zinazohusu rasilimali watu, wasimamizi wa mifumo ya mawasiliano, wanasheria na wahasibu.

Tangazo hilo limesisitiza kuwa wale wanaohisi kuwa na mahitaji maalumu wanapaswa kujieleza kwenye barua zao ambazo zinawezwa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza.

Waombaji wameelekezwa kutuma maombi yao kupitia mtandao wa portal.ajira.go.tz au pia kutembelea mtandao wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.