Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mume amchinja mke hadi kufa, wivu wa mapenzi watajwa

Muktasari:

Watu wawili wamefariki dunia mkoani Mara katika matukio mawili tofauti likiwemo la mume kumchinja mke wake kutokana na ugomvi wa kifamilia na kupelekea Jeshi la Polisi mkoani kuwashikilia watu wawili wakihusishwa na mauaji hayo.

Musoma. Watu wawili wamefariki dunia mkoani Mara katika matukio mawili tofauti likiwemo la mume kumchinja mke wake kutokana na ugomvi wa kifamilia na kupelekea Jeshi la Polisi mkoani kuwashikilia watu wawili wakihusishwa na mauaji hayo.

Kuhusu tukio la kwanza Kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Daniel Shillah alisema lilitokea katika Kijiji cha Manchimweru wilayani Bunda, Novemba mosi ambapo mwanamke aliyejulikana kwa jina la Shida Shop (25) aliuawa kwa kuchinjwa na mume wake Masunga Ndilama (25).

Alifafanua kuwa kabla ya tukio hilo mwanume huyo alimuomba mke wake waende kijiji cha jirani kwa matembezi ya kawaida lakini kabla ya kufika katika kijiji hicho mwanaume huyo alimchinja mke wake na kufariki dunia.

“Kabla hawajafika katika kijiji hicho walipita kwenye pori lilipo katika kijiji cha Manchimweru na hapo hapo akatoa kisu na kimshika mke wake kisha kumchinja hadi kumuua,” alisema Kamanda Shillah

Alisema baada ya kufanya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alijikata sehemu zake za siri kwa sababu ambayo haijajulikana.

Baada ya tukio hilo mwanamume huyo alikamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika na hivi sasa amelezwa hospitalini kwa ajili ya matitabu.

Alisema kuwa chanzo cha ugomvi wa wanandoa hao ni mwanamke huyo kuchukua vitu vya ndani na kuhamia Bunda kutoka katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi walipokuwa wakiishi, kabla ya mume huyo kuhamia Zanzibar.

Alieleza kuwa awali wanandoa hao walikuwa wakiishi Mpanda baadaye mume alikwenda Zanzibar kutafuta maisha ambapo alikaa kwa muda mrefu na mke akaamua kuhamia wilayani Bunda alikozaliwa akiwa na vitu vyote vya ndani bila mume wake kujua.

Alisema baada ya mume kurudi Katavi akitokea Zanzibar alipewa taarifa kuwa mkewe alihamia Bunda ndipo naye alipofunga safari hadi Bunda na kumuomba mkewe warudi Katavi.

Kamanda alisema baada ya mume kushindwa kumshawishi mkewe, alijifanya kukubaliana na mke kuishi Bunda.

Kumbe ana mpango tofauti, siku hiyo alimwambia mke wake watoke kwa matembezi huku akiwa amejiandaa kumuua mke wake na alibeba kisu ambacho alikitumia kumchinja.

Katika tukio lingine Shillah alisema polisi wameendelea kumshikilia Nchagwa Sasi (18) kwa tuhuma za kumuua Kegoko Kitaro baada ya kuchukizwa na kitendo cha kumfukuza kutoka kwenye sherehe ya harusi kwa kukosa zawadi.

Kitaro alikuwa mwenyekiti wa kamati ya zawadi kwenye harusi iliyofanyika kijiji cha Merenga Wilaya ya Serengeti na aliamua kumfukuza mtuhumiwa kwenye sherehe baada ya kubaini hakuwa na zawadi kinyume cha makubaliano ya wana kamati.

“Baada ya sherehe kumalizika, mtuhumiwa alikutana na marehemu na kuanza kumhoji kwanini alimfukuza kutoka kwenye sherehe ndipo mzozo ulipoibuka. Katika mzozo huo, mtuhumiwa alimchoma mwenzake shingoni na kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo chake papo hapo,” alisema Kamanda Shillah